Vile vile ibara inaainisha hadhi na haki sawa za Nchi Washirika. b. Madhumuni na Lengo Madhumuni ya Ibara ni kutambua kuwepo kwa Nchi Washirika zinazounda na kuipa uhalali wa Jamhuri ya Muungano. Lengo la Ibara hii pia ni kuainisha hadhi na haki ya kila Nchi Mshirika ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia usawa na ukweli kwamba Muungano huu ni wa hiari. Hadhi na haki inayotajwa hapa siyo ya usawa wa mahitaji na kuchangia bali ya usawa na uhuru kwa maana kuwa kila moja ilikuwa nchi kamili ilipojiunga na Muungano. c. Sababu za Mapendekezo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua Nchi Washirika katika Ibara ya 4, 34, 64, 102. Aidha Ibara ya 151 inatamka kuwa Tanzania Bara maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Tanganyika na Tanzania Zanzibar maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa ni eneo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Hivyo moja ya sababu ya Ibara hii ni kuendeleza dhana hii ya kihistoria. Sababu nyingine ni kuweka wajibu wa msingi wa kuleta maendeleo na usatwi wa watu wa kila upande wa Muungano chini ya mamlaka ya Nchi Mshirika husika. Aidha, sababu ya Ibara hii pia ni kuitikia madai ya wananchi kutaka utambulisho rasmi na wa wazi kwa kila Nchi Mshirika katika Muungano. Takwimu za maoni ya wananchi kuhusu suala hili zimo katika Ripoti ya Tume, “Takwimu za Ukusanyaji wa Maoni ya Wananchi Kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaâ€, Sura ya Nne, Eneo la Muungano, hoja 4.2.2, Hadhi za Washirika wa Muungano kwa Sehemu Mbili za Muungano. Ibara ya 65: Mamlaka ya Nchi Washirika a. Maudhui ya Ibara Ibara hii ya Rasimu ya Katiba inafafanua Mamlaka ya Nchi Washirika katika utekelezaji wa mambo yote yasiyo ya Muungano yaliyo chini ya mamlaka zao. Ibara inabainisha kuwa katika utekelezaji wa mamlaka hayo, Nchi Mshirika itazingatia misingi ya ushirikiano baina yao. Aidha, Ibara inaelekeza kuwa Nchi Washirika zinaweza kuanzisha mahusiano au mashirikiano yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo yasiyo ya Page 72 59 Muungano na zinaweza kuomba ushirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano ili kufanikisha suala hilo. Ibara vile vile inaeleza kuwa katika kutimiza mamlaka ya Nchi Washirika kwenye masuala ya kikanda na kimataifa kila moja peke yake au kwa kushirikiana na Jamhuri ya Muungano, zitafuata utaratibu uliowekwa kwenye Katiba kupitia vyombo vilivyomo ndani ya Katiba hii. Vyombo hivyo ni Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali na Mawaziri Wakaazi, pamoja na sheria itakayotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa madhumuni hayo. b. Madhumuni na Lengo Madhumuni ya Ibara hii ni kuainisha mamlaka na haki ya kila Nchi Mshirika wa Muungano ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano; kuziwezesha Nchi Washirika kusimamia na kutekeleza mambo yasiyo ya Muungano katika maeneo yao; pia kuziwezesha kikatiba Nchi Washirika wa Muungano kutekeleza masuala ya ushirikiano wa kimataifa katika maeneo yasiyo ya Muungano na kuepusha migongano inayoweza kutokea kati ya Nchi Washirika na Jamhuri ya Muungano au Washirika wa Muungano wenyewe kwa wenyewe. c. Sababu za Mapendekezo Katiba hii inabainisha kuwa Nchi Washirika wa Muungano zitakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya muungano yanayohusu Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa juu ya mambo yote yasiyo ya muungano yanayohusu Zanzibar. Kwa mantiki hiyo, Nchi Washirika wa Muungano zitakuwa na mamlaka kamili ya kutekeleza mambo yote yasiyo ya Muungano ikiwa ni pamoja na kuanzisha ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kuhusiana na mambo hayo kwa mujibu wa Katiba. Aidha, Rasimu inapendekeza Nchi Washirika kuruhusiwa kuomba ushirikiano kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha suala hili. Jukumu la Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika suala hili ni kufanikisha utekelezaji wake. Mapendekezo haya yamezingatia kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni taifa moja lenye dola moja. Aidha, yanatambua hadhi na haki sawa za Nchi Washirika wa Muungano na kuweka utaratibu utakaorahisisha na kuharakisha juhudi za kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi katika Jamhuri ya Muungano. Mapendekezo haya pia yanaweka msingi wa mshikamano (Solidarity Principle) baina ya Nchi Washirika. Moja ya sababu za mapendekezo haya ni hoja kwamba Zanzibar inastahili kuwa na mamlaka ya kujihusisha na masuala ya kimataifa ili kukuza maslahi yake. Inadaiwa kuwa hali ya sasa ambapo masuala yote ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ni masuala ya Muungano, Zanzibar inapungukiwa na fursa za kujistawisha kimaendeleo. Hivyo, imeonekana haja ya kutenganisha masuala ya mambo ya nje (International Relations) nay ale ya ushirikiano wa kimataifa (International Co operation) ili kutoa fursa pana kwa Nchi Washirika kushughulikia ustawi wa kimaendeleo wa maeneo yao. Sababu nyingine ni kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitakuwa ya kwanza duniani kuruhusu washirika wake kuwa na mashirikiano ya kimataifa. Nchi za Marekani, Page 73 60 Ujerumani, Canada, Austria na Uswisi zimeruhusu washirika wao wa Muungano kujihusisha na masuala ya ushirikiano wa kimataifa kwa njia mbalimbali kama vile kwenye masuala ya mikataba, kufanya ziara, kutafuta na kutoa misaada na kuwasiliana na wadau mbalimbali wa kimataifa. Washirika wa Muungano wamekuwa wakiendesha shughuli za uhusiano wa kimataifa moja kwa moja kwa hadhi zao kama Washirika wa Muungano kwa mambo yaliyopo kwenye mamlaka zao na siyo shughuli za asili za nchi huru kama vile ulinzi na usalama (strategic and security matters). Mara nyingi masuala hayo yamekuwa yakihusiana na masuala yanayo wakabili katika maeneo yao ya utawala kama vile utamaduni, mazingira, biashara na masuala ya maendeleo kwa jumla. Ibara hii isomwe pamoja na Ibara za 66 na 67. Ibara ya 66: Mahusiano kati ya Nchi Washirika a. Maudhui ya Ibara Ibara hii ya Rasimu ya Katiba inaweka misingi ya ushirikiano na mashauriano baina ya Nchi Washirika wenyewe kwa wenyewe au kati yao na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa shughuli zao kwa lengo la kukuza na kulinda maslahi ya taifa na maendeleo ya wananchi. Ushirikiano na mashauriano hayo ni katika mambo ya uongozi, utawala, vyombo vya uwakilishi na mahakama, na yatekelezwa kwa kuzingatia na kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya taifa. b. Madhumuni na Lengo Ibara hii inalenga kuweka utaratibu wa kikatiba utakaowezesha usimamizi na ushirikiano baina ya Nchi Washirika wenyewe, na kati yao na Jamhuri ya Muungano. Lengo jingine ni kukuza umoja na mtangamano wa kitaifa kwa kuzingatia maslahi ya taifa na ustawi wa wananchi. Kuwezesha Nchi Washirika kutambua na kuhamasisha wananchi wao kutumia fursa zilizopo katika pande zote mbili za Muungano na shughuli hizo zikifanywa na wananchi wenyewe. c. Sababu za Mapendekezo Katika nchi yenye mfumo wa shirikisho au Muungano, Nchi Washirika na Serikali ya Muungano zinawajibika kushirikiana na kushauriana ili kuweka misingi ya kuwahudumia wananchi wote kwa usawa, haki, ulinganifu na uwiano katika masuala ya ustawi wa jamii na maendeleo. Kwa mujibu wa Rasimu hii, vyombo vya kushughulikia suala hili ni pamoja na Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali na Mawaziri Wakaazi. Sababu ya mapendekezo haya ni kuepusha migongano katika uendeshaji wa shughuli za dola na serikali kwa kuwa na vyombo na taasisi vinavyosimamia na kuratibu uhusiano na ushirikiano wa pande husika. Page 74 61 Sababu nyingine ni kukuza na kulinda maslahi na ustawi wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa ujumla wao lakini bila ya serikali za Nchi Washirika kuingiliana. Ibara ya 67: Mawaziri Wakaazi a. Maudhui ya Ibara Ibara hii ya Rasimu ya Katiba inaanzisha nafasi za Mawaziri Wakaazi watakaoteuliwa na nchi zao na kua na ofisi makao makuu ya Muungano. Ibara pia inaainisha majukumu yao ambayo ni kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu ushirikiano au mahusiano ya kimataifa; na kuwa kiungo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Nchi Washirika na baina ya Nchi Washirika wenyewe kwa mambo ya Muungano na yale yasiyokuwa ya Muungano. b. Madhumuni na Lengo Madhumuni ya Ibara hii ni kuweka chombo cha kikatiba chenye dhamana ya kushughulikia mambo yote yasiyo ya Muungano ili kuunganisha, kuratibu na kusimamia shughuli za kila siku. Ibara pia inalenga kujenga utamaduni wa kiutawala utakaoleta ukaribu na ushirikiano katika Jamhuri ya Muungano na hivyo kujenga imani juu ya maamuzi yanayofanywa katika ngazi hiyo. c. Sababu za Mapendekezo Moja ya sababu za mapendekezo haya ni kurahisisha uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za Nchi Washirika katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Vilevile ni kufuata uzoefu wa baadhi ya nchi zenye muundo wa shirikisho wa kuwa na Mawaziri Wakaazi au Ofisi za Uwakilishi wa kila Nchi Mshirika wanaoratibu na kusimamia mambo ya shirikisho na maslahi ya Nchi Washirika ndani ya Muungano. Mfano wa nchi hizo ni Ujerumani na Canada. Jumuia ya Umoja wa Ulaya nayo pia ina utaratibu kama huo. Aidha, sababu nyingine ni kuendeleza utaratibu ulioanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuwa na Ofisi Jijini Dar-es-Salaam ambayo ni Makao Makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 68: Mamlaka ya Wananchi a. Maudhui ya Ibara Ibara hii ya Rasimu ya Katiba inasema kuwa wananchi ndio chimbuko kuu la mamlaka ya nchi. Hivyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na chombo kitakachopewa mamlaka na Katiba. Aidha, Nchi Washirika zitapata mamlaka kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka chini ya Katiba zao. Serikali za Nchi Washirika, katika kutekeleza mamlaka yao, zitawajibika kustawisha mamlaka ya wananchi kwa kugatua madaraka kwa Serikali za Mitaa zitakazoanzishwa kwa mujibu wa Katiba zao. b. Madhumuni na Lengo Madhumuni ya Ibara hii ni kutambua ukuu wa wananchi kikatiba na kuziwajibisha mamlaka zote kwa wananchi. Page 75 62 c. Sababu za Mapendekezo Sababu ya mapendekezo haya ni kutambua kuwa mamlaka kuu ya dola na nchi ni wananchi na sio watawala au vyombo vya serikali na vyote hivyo viko chini ya wananchi kwa mujibu wa katiba. Katika historia ya nchi nyingi za Kiafrika dhana ya ukuu wa wananchi ilififishwa na badala yake ikakuzwa dhana ya ukuu wa utawala na vyombo vya serikali. Mapendekezo haya ni kurudisha dhana ya ukuu wa wananchi katika uendeshaji wa nchi. Ili kuweza kutekeleza dhana ya Mamlaka ya wananchi ni vyema Katiba ikaanisha vyombo vya kikatiba kama uwepo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambavyo ndivyo vyenye uwakilishi wa wananchi moja kwa moja na ndivyo vyenye wajibu wa kutoa huduma moja kwa moja kwa wananchi. Sababu ya mapendekezo ni kuendeleza maudhui ya Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Ibara ya 9 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 zinazotambua mamlaka ya wananchi ingawa katika utekelezaji bado mwelekeo umekuwa zaidi kwenye mamlaka ya watawala na vyombo vya serikali. Muhimu zaidi mapendekezo haya ni kukubaliana na maoni ya wananchi waliotaka Katiba ionyeshe wazi kuwa Mamlaka ya nchi yanatokana na wananchi wenyewe na kwamba, vyombo vya Serikali vimewekwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia. Ibara ya 69: Wajibu wa Kuulinda Muungano a. Maudhui ya Ibara Ibara hii ya Rasimu ya Katiba, inaweka wajibu kwa kila raia, viongozi wakuu wenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar kuulinda, kuuimarisha na kuudumisha Muungano. Kwa hiyo kila kiongozi Mkuu kabla ya kushika madaraka yake ataapa kuutetea na kuudumisha Muungano. Aidha, Ibara pia inaainisha hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa atakayeshindwa kutekeleza wajibu huu. b. Madhumuni na Lengo Madhumuni ya Ibara hii ni kutambulisha kuwepo kwa Muungano katika maisha ya taifa letu na kujenga uzalendo na mshikamano; na hivyo, kuuthamini, kuulinda na kuutetea Muungano huo wa hiari baina ya raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia umoja wao, udugu, urafiki na mahusiano yao ambayo yana uhusiano ya muda mrefu. c. Sababu za Mapendekezo Sababu za kuwepo kwa Ibara hii ni kusisitiza wajibu wa viongozi wenye dhamana ya juu ya uongozi wa nchi kuuheshimu na kuusimamia Muungano kwa kila hali ili kuuendeleza, kuuhuisha na kuudumisha. Vilevile ni kutambua kuwa Muungano huu wa hiari ni wa wananchi wenyewe na viongozi wao lazima wautii na wauheshimu. Uzoefu umeonyesha kuwepo kwa uvunjaji Page 76 63 wa Katiba kwa viongozi kukubaliana masuala kadhaa bila ya kuwashirikisha wananchi kwa makusudi au vinginevyo. Page 77 64 SURA YA SABA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO SEHEMU YA KWANZA SERIKALI, RAIS, MAKAMU WA RAIS NA BARAZA LA MAWAZIRI (a) Serikali Ibara ya 70: Serikali ya Jamhuri ya Muungano a. Maudhui ya Ibara Ibara hii ya Rasimu ya Katiba inaelezea kuwepo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakayoundwa na Rais, Makamu wa Rais na Mawaziri ambao watahusika na utekelezaji wa Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hifadhi ya Katiba. Aidha, inampa uwezo Rais wa kutekeleza majukumu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yeye mwenyewe au kwa kukasimu madaraka hayo kwa Makamu wa Rais au watu wenye
pata zaidi katiba ndani ya google.com
ikishilikiana na ayubuhenry.blogspot.com