HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 6

HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 6

HUKUMU YA HAKI
SEHEMU YA..6
Mtunzi Ayubu Henry

ILIPOISHIA....

Jesika alimuangalia babayake alie kuwa ameshika  usukani vyema.. binti huyu aligundua kuwa hakika baba yake alikuwa akimaanisha kile alicho kuwa akikiongea.
"Nilazima Esilomu nimsaidie kwa tatizo hili aliro naro, kwanza ni ndugu yangu ni mtoto wa dada yangu ila harafu niwajibu wangu kusimamia sheria lazima haki itendeke siwezi kumuacha kabisa afe nikiwa naona ni mtu  wa muhimu kwangu, nadhani nikifanya mchakato kesho asihamishwe na kesho kutwa asinyongwe basi nitakuwa nimefanya vizuri itanibidi nifanye uchunguzi kuhusu maisha ya hawa watu wawili ndipo nitakapo kuwa nimempa uhuru Esilomu kinyume na hapo atanyongwa tuu, siwezi kuruhusu hili dada yangu alikwenda ila mwanae hawezi kwenda kingali nipo hai..". jaji alikuwa akijiwaza huku akiwa anaendesha gari kwasi kuelekea ikuru kwa raisi wa jamhuri ya muuangano wa tanzania.


ENDELEA.......

Munamo saa sita na dakika ishirini na mbili Jaji Edisoni alifika  ikuru kwa mheshimiwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania mheshimiwa  Gabrieli Musa.
walipokelewa na walinzi pale inje ya geti kubwa walinzi wale waliwasongeza mpaka geti la pili katika geti hili walipokelewa na vijibaba ambavyo kwa kawaida ungesema ni wapambanaji wa ulingoni au ungesema ni wakaza misuri.
"Samahani walinzi vipi kweri nimemkuta mheshimiwa?" jaji aliuliza kwakuwa alikuwa anaheshimika alijibiwa tofauti na watu wanao kuja nakuuliza kisha wasijibiwe.
"ndiyo yupo" ilikuwa sauti nzito kutoka kwa mrinzi mmoja wa mheshimiwa raisi.
"vipi yumo ndani au kule nje sehemu ya kupumuzikia" jaji aliuliza kutaka kupata ufafanuzi wa kina kuhusu alipo kuwa raisi.
"yupo kule bustani kwahiyo ukimtaka nenda kulekule" mlinzi yule alijibu.
"sawa nashukuru,   Jesika Twende".
waliongozana mpaka wakafika bustanini
"karibu.. .....karibu sana, jaji vipi bwana za nyumbani huko?" Mheshimiwa Gabrieli aliwakaribisha
"asante sana na nimesha karibia , huyu unae muona hapa ni mwanetu yule mdogomdogo wa siku zile sasa amekua siyo mdogo tena" jaji alisema.
"anaitwa nani nani.....nani Jesika?" raisi  alihoji.
"ndiyo kabisa" kabla jaji  hajamaliza Jesika akamuamkia raisi "shikamo mzee?" jesika aliamkia
"marahaba!!!! haujambo mama?" raisi aliuliza
"mimzima kabisa mungu anasaidia, maana ni wengi walio tamani kufika siku ya leo lakini hawaja weza ila mimi bado nipo shukulani kwake alie juu" Jesika alisema.

muda mchache ulipita baada ya jaji kufika ikuru, alionekana ana kitu cha kuongea lakini alisitasita kusema.
Raisi akaanza "Ndiyo jaji majukumu ya kifamilia yakoje na vipi nasikia unashikilia vyema sheria, ila nikupongeze kwa juhudi zako za kusaidia tanzania maana bila mahakama hakuna sehemu nyingine penye mamulaka ya kuhukumu ni mahakama tuu, hakika nyie ni wa mhimu katika kusimamia sheria, tunahitaji watu kama nyie" Gabrieli hakumalizia akaambiwa na mmoja wa walinzi wake kuwa simu yake kunamtu amepiga aliomba musamaha kwa jaji na kutaka kuzungumza na mtu simuni, ali toka pale walipo kuwa wame kaa na kuzungumuza na mtu yule aliekuwa amempigia.

"sasa Jesika nakuomba unisubilie hapo nje kuna mambo ya muhimu tunayo taka kuongea mimi na raisi hasa kuhusuEsilomu kwahiyo naomba unisubiri hapo nje, muda si mrefuvnitakuja sawa?" Eddi alimwambia Jesika na baada ya muda wa dakika nne raisi alirudi
"Eddi samahani kwa kuningojea alie kuwa amepiga ni mtu wa mhimu sana hivyo nakuomba ladhi kwa kujari simu na kukuacha hapa!" raisi alisema.
"hakuna tatizo mkuu wala usinihofie kabisa mkuu,"Edisoni alisema
"sawa, ehe vipi lakini unatumia kinywajigani?" mheshimiwa raisi aliuliza.
"aaaa hapana mkuu sijisiki kupata kinywaji". jaji alijibu.
"aaaaaaaaa wewewewe, hapa ni nyumbani Eddi jisikie upo kwako kabisa tena jisikie uko nyumbani kijana wangu!!!" Raisi aliongezea.
"Nashukuru sana mkuu".Eddi alisema..

"kwani vipi ndugu kuna tatizo mpaka hata kinywaji usitake??" Raisi aliuliza.
"Ndiyo lipo" eddi alijibu
"lipi tena".
"nikubwa kiasi, lakini nimekosa sehemu ya kwenda nikaamua nije kwako angalau kutafta msaada na nadhani hapa ni sehemu sahihi". Eddi alisita kido harafu akaendelea.

"mkuu kwakweri sina mtu alieko juu mwenye kunisaidia kwa hili."
"sawa wewe sema hapa ni nyumbani na kama nilivyo tangulia kusema ni kwamba jisikie uko nyumbani, kuwa huru kabisa kijana wangu,
wewe ni moja kati ya vijana wanao tegemewa katika ujenzi wa taifa." Raisi alisema huku Jaji Eddi akijianda kusema lililo mleta pale japo kuwa bado alikuwa na kigugumizi kikubwa kwa kuhofia kuwa Raisi asinge kubari ombi lake  kwa sababu upana wa kesi ya Esilomu ni mkubwa mpaka ilimtia shaka kubwa sana alipo kuwa anakumbuka kwamba alie kufa ni waziri mkuu wa mambo ya ndani na makamu wa raisi, tena makamu wake huyuhuyu raisi alieko madarakani.
alijikaza mwisho akasema.
"mheshimiwa sikupenda kukupotezea muda, lakini nitatizo lenye upana mkubwa sana ila ninakuomba unisikilize kisha uangalie wapi pa kunisaidia."
alinyamanza kidogo kisha akaendelea.

"mimi naitwa Edisoni Mwasera nililelewa na mtu ambae si baba yangu, baba yangu na mama yangu walifariki takiribani miaka 28 iliyo pita, niliishi na dada yangu yaani anae nifata kuzaliwa, familia ya mzee Mwasera ilibahatika kupata watoto wawili tu yaani mimi na dada yangu.
maisha yalitubana sana  mimi na dada yangu baada ya baba na mama kufariki tukaamua kusambaa kwenda kutafta musaada sehemu nyingine, mimi nilibahatika kupata nafasi ya kuishi na mkuu wa mkoa wa kipindi kile
lakini mdogo wangu yaani huyo binti siku moja alinitumia ujumbe yaani barua fupi ikisema yeye alipata kazi ya kuweza kumdu maisha aliyo kuwa anaishi, alicho kidai ni kwamba alipata mtu wa kumuajiri kwenye hoteli moja kule Arusha, alipelekwa na yule mtu kumbe masikini yule mtu hakuwa na roho nzuri
alimpeleka na kuanza kumuuza dada yangu akawa anatumikishwa kama mnyama,
alikuwa anauzwa kwa wanaume watumie mwili wake na mtu alie kuwa akimwajiri alihakikisha kwamba anajipatia masirahi kupitia mwili wa dada yangu.
mwisho wa siku alibahatika kupata mtoto ila baada ya kupata mtoto dada yangu hakumjua baba yake yule mtoto kwa sababu alikuwa ametembea na watu wengi kwahiyo ilikuwa ngumu kumjua baba harisi wa mtoto yule ni nani.
Baada ya siku chache dada yangu ikasadikika kafa na mtoto yule akakosa msaada japo kuwa alilelewa na mzee mmoja ila hakumkidi mahitaji yake ya msingi kama vile kumsomesha ne mengine mengi mwisho wa siku akajiingiza katika vikundi vinavyo sambaza bangi na aina nyingine ya madawa ya kulevya, kazi hii ameifanya chini ya mtu mmoja ambae mwisho alimuzurumu lakini kijana huyu baada ya yote hayo aliamua kulipiza, moja alianzia na alie muua mama yake yaani dada yangu na mwisho akamuua mtu alie mzurumu pesa baada ya kufatilia malipo na kukosa." jaji alionekana amemaliza ila chozi lilimtoka alipo kuwa akiwaza mateso ambayo dada yake aliyapata kama kila siku lazima atumiwe na wanaume watano au mpaka saba tena kikatili kwa kulazimishwa na pia kila siku ilimbidi afanye kazi hiyo ambayo alikuwa analipwa kidogo sana au asilipwe kabisa hakika alitoa chozi.

"pole sana Eddi kwa matatizo yaliyo kukumba na kukufanya uumie tena uteseke, eddi hii nilazima binadamu apitie kwenye maisha yake unaweza kudhani uko peke yako pindi unapo patwa na tatizo unadhani dunia yote umeumbiwa wewe tuu lakini hata mafundisho ya biblia inafundisha tuwe na uvumilivu, kwa hiyo usijari sana, mimi mpaka nafika hapa nimepitia mengi mno tena mengi sana ambayo leo hii nikikwambia huwezi kuamini ndiyo maana leo mimi watu wenye matatizo nawasaidia ni kwa sababu najua niliko toka na laiti viongozi watakao fata na waliomo madarakani wangeliona hili wakaamua kutumia pesa zao kwa ajiri ya kusaidia na siyo kwa ajiri ya siasa hakika tunge endelea. Lakini kama raisi wa nchi hawaniungi mkono napojaribu kutafta msaada wa watu ambao hawajiwezi hakika hatuwezi kufika". Gabrieli raisi mwenye busara alimweleza Edisoni.

dakika chache kupita Raisi akauliza "sasa Edisoni nikusaidie wapi, kweri umesema tatizo lakini je unataka msaada gani kutoka kwangu.?"
Edisoni akaangalia chini nakusema "mkuu huyu kijana ninae mzungumzia kwa sasa yupo jera amesubiri kunyongwa, alie toa hukumu ni mimi mwenyewe lakini kwa shinikizo la viongozi wa juu ndo maana nikatoa hukumu ile".
"jina lake nani?" Raisi aliuliza kutaka kumjua.
"ni huyu Esilomu Ngware"
"huyu alie muua makamu wangu au?" raisi aliuliza
"ndiyo na mama yake ni binti mmoja alie kuwa dada yangu nae anaitwa Penina Mwasera" jaji alisema.
"weee Penina Mwasera?" raisi akauliza
"ndiyo Penina Mwasera ni dada yangu" jaji alijibu.
"etii Penina Mwasera?? Penina huyuhuyu ninae mjua au? ha!
haiwezekani kabisa Penina Mwasera eti ni dada yake na Edisoni?" Raisi aliwaza huku moyo ukimuenda mbio.
"kwani unamfahamu Penina Mwasera?? binti huyu alisha kufa siku nyingi zilizo pita". jaji aliuliza na kumueleza Raisi.
"aa!a! poleni sana na pole sana kwani unataka nifanyeje ili kukusaidia?" raisi aliuliza.
"ninacho taka nikwamba Esilomu asinyongwe bali kesi isubiri ukweri na mwisho uandaliwe huo ukweri ufikishwe mahakamani ili ionekane haki iko wapi je anyongwe Esilomu au aachiwe!!."
"Edisoni nimekuelewa najua cha kufanya wewe nenda nyumbani nitazuia asinyongwe na baada ya kuzuia asinyongwe tutaangalia jinsi nyingine ya kufanya".
"siamini kabisa" jaji alisema.
" wewe amini sawa jaji?" Raisi alisema japo kuwa Jina la Penina liliendelea kumfanya ashindwe na mazungumzo akawa anaongea kwa kukata kata maneno.
"sina shukurani ya kukupa mheshimiwa ila mungu atakurudishia ni yeye ampae yeyote kitu chochote tumuombacho" jaji alishukuru hakuamini kabisa alihisi ni ndoto aliyo kuwa anaota wakati ule
"wewe nenda nyumbani nadhani kesho asubuhi utasikia taarifa kwenye redio hii ya tanzania au tbc1 na vyombo vingine kwenye yaliyo jili na nadhani wandishi wa habari watakuja kwako kupata mawili matatu kutoka kwako". raisi alisema.
jaji alishukuru nakuagana na mheshimiwa raisi tayari kuanza safari kurudi nyumbani.

"Haiwezekani eti Penina Mwasera ana mtoto tena ni mtu alie saidia kuiokoa tanzania he! mbona sikulijua hili mapema ngoja nifatilie kwanza sababu  haiwezekani". raisi alikuwa anajiwaza huku akieleka sehemu ambapo magari yana pakiwa na kufunguliwa mlango akamwambia mwendesha gari
"naomba twende Nyumba namba H2029 balabala namba 32  fanya haraka". mwendesha gari alitoa gari kwa kasi kuelekea huko ambapo raisi amepahitaji kwenda.
mara nyingi huenda kwenye nyumba hii kwa kificho kikubwa asionekane na huenda na mlinzi mmoja tu.
"Siamini anacho kisema jaji kama kinaukweri lakini nitajua tu ukweri uko wapi."alikuwa akijiwaza na kuona gari kama harikimbii sana ili wawahi kufika.


ITAENDELEA....
TUKUTANE SEHEMU IJAYO
LIKE NA COMMENT ILI TUWE WOTE.