HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 7

HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 7

HUKUMU YA HAKI
SEHEMU YA..7
Mtunzi Ayubu Henry

ILIPOISHIA....

Haiwezekani eti Penina Mwasera ana mtoto tena ni mtu alie saidia kuiokoa tanzania he! mbona sikulijua hili mapema ngoja nifatilie kwanza sababu  haiwezekani". raisi alikuwa anajiwaza huku akieleka sehemu ambapo magari yana pakiwa na kufunguliwa mlango akamwambia mwendesha gari
"naomba twende Nyumba namba H2029 balabala namba 32  fanya haraka". mwendesha gari alitoa gari kwa kasi kuelekea huko ambapo raisi amepahitaji kwenda.
mara nyingi huenda kwenye nyumba hii kwa kificho kikubwa asionekane na huenda na mlinzi mmoja tu.
"Siamini anacho kisema jaji kama kinaukweri lakini nitajua tu ukweri uko wapi."alikuwa akijiwaza na kuona gari kama harikimbii sana ili wawahi kufika.

ENDELEA...................

"Jesika unajua mpaka sasa siamini kinacho endelea, yaani Raisi amekubari ombi langu hakika maajabu". Edisoni alimweleza mwanae Jesika huku akiongeza mwendo ili kuzipita gari tatu zilizo kuwa mbele yake.
"kwahiyo hajaleta hata upingamizi wowote bali amekukubaria?" Jessi aliuliza
"hapana hajaleta upingamizi wowote  mimi nime mweleza kila kitu lakini baadae hajakataa ombi langu ameniambia kuwa hili atalizuia kwanza asinyongwe mtu huyu na pia lingine ameniambia kuwa inaweza kutokea waandishi wa habari wakataka kuhoji, kwanini hajanyongwa? lakini wakija kwangu basi sita hangaika bari nitakacho kifanya ni kuwaambia kwamba kuna mambo mengi ambayo yamelazimu kusitishwa kunyongwa mtu huyu." jaji alisema.
"sawa baba lakini baada ya hayo yote unataka ufanye nini kwa sababu ukizingatia kesi hii ni kubwa hawezi kuachiwa hivihivi lazima atanyongwa sasa wewe unalipi la kufanya" Jesika aliuliza.
muda kidogo ulipita jaji akijihisi furaha kubwa moyoni alicho kijibu baada ya Jessi kumuuliza ni "Jessi mimi sina utaalamu wa upelelezi nikimaanisha sikusomea upelelezi bari nilisomea sheria sasa kwangu ni ngumu sana kufuatilia na kupata ukweri wote, hii ni kwasababu tuu kuhitaji kuthibitisha kuwa walio kufa walikuwa na hatia na siyo huyu anae enda kunyongwa bali wale walio kufa," jaji alinyamanza na kuendelea
"wale watu ni waharifu sasa ili kuthibitisha ukweri wote lazima apatikane mpelelezi alie bobea ili afanye uchunguzi wa maisha waliyo kuwa wanaishi hawa watu, ukweri wote ukiwa wazi basi Esilomu hana hatia lakini bila kupata ukweri wa jambo hili basi niwazi Esilomu bado atakufa tu ila kumusaidia ni kutafta ukweri wa maisha ya hawa watu wawili yaani Ishimael Shemley na Fabiano Andrew
tukisha pata uharisia wao basi kesi imeisha lakini nibaada ya kumpata mchunguzi anae weza kubaini maisha ya hawa watu basi bado kazi ipo ila najua mungu yupo  atatusimamia  kama alivyo musimamia Musa kuwaongoza wana wa Isirael basi nasi atatuongoza kumpata mchunguzi.
tunahitaji mchunguzi kwa sababu hawa watu walifanya kificho kikubwa ili wasijulikane lakini naamini kwa ushirikiano tunaweza kuwa gundua." jaji alikatishwa kuongea baada ya simu yake kupigiwa
"haloo!" sauti ya upande wa pili ilisikika baada ya jaji kupokea simu.
"halooo" jaji akaitikia
"mko wapi mbona mda mrefu hamjarudi vipi kunatatizo?" Bi Heleni aliuliza
"hapana tupo njiani tunakuja usijali sawa!!"
"ok nawasubiri" Heleni alisema
na kukata simu.
"ni mama!" alimwambia Jesika
"ok sawa haina shida hii kwani situnaenda?" Jesika alisema
.

******
 
.*
*
*
Baada ya dakika kumi na tano Gabrieli raisi wa jamuhuri ya mungano wa tanzania akafika kwenye nyumba  moja kubwa iliyo zingirwa na ukuta mrefu kwenda juu na mpana.
ni nyumba yenye hadhi kubwa hapa Dar es salaamu wengi wanadhania hakuna mtu anae ishimo.
ndani ni seheme nzuri palipo pambwa na maua ya kupendeza ambayo yalipafanya paendelee kung'a kwa uzuri wa kipeke sana.
Mwendesha gari alienda akalisimamisha sehemu maalumu ya kusimamisha magari
Raisi hakusubiri afunguliwe mulanga alijifungulia akaanza safari ya kuingia ndani ya nyumba hii ambayo kwa sasa ilikuwa kimya sana japo kuwa kunandege wadogowadogo walio kuwepo mahari hapa wakiendelea kutoa sauti zao.
alitembea kwenye velanda ndefu na kufika sebreni lakini hapakuwepo mtu yeyote mahari pale kama siyo ndege aina ya kasuku.
alienda moja kwa moja kwenye chumba kimoja kilicho kuwa kimefungiwa kwa ndani
"ali gonga gonga kwa kutumia mkono wake pale mlangoni mara tatu kisha akasema "Ni mimi fungua mlango"
"nakuja kufungua" sauti nzuri ya mwana mke ilisikika mre chumbani
mlango ukafunguliwa
"karibu sana, vipi mbona hauja nitaarifu kua unakuja" binti huyu alisema.
"samahani sana Penina" Gabriel alisema kwa kumuomba msamaha
"Usijari karibu ndani"penina alisema.
"vipi kuna mapya huko? mbona umefika gafra namna hii? Penina aliuliza.

kimya kidogo kilipita raisi akasema "Penina kwanza naomba kabla sijaongea nikuulize"
"uliza tu usijari". penina alijibu.
"Unamjua Esilomu?" Gabri
aliuliza, swari hili lilimfanya ashindwe kuongea kitu akabaki ameduwa.
"Penina nauliza tena Je,unamfahamu Esilomu?" Gabri aliuliza tena sauti hii ilionesha amedhamilia kwa kile alicho kuwa akikiongea.
"Kwahiyo umenileta tanzania kwakutaka niishi kwa huzuni? au umenileta tanzania kufanya nini maana kila kitu unacho kifanya ni kuniumiza tuu sasa ndo nauliza umeamua kuniumiza au?" penina alisema huku macho yake yakianza kutokwa na machozi.
"Penina nauliza tena kwa mara ya mwisho je,unamjua Esilomu? nijibu kama unamjua". raisi aliuliza tena
"My love naomba usikie mimi ni binti nilie ishi maisha ya shida sana miaka ishirini na nane iliyo pita nilikuwa naishi na kaka yangu ambae nilimpenda sana alikuwa anaitwa Edisoni Mwasera tuliishi sisi tu wawili baada ya wazazi wetu kufariki, hatukua na msaada ila siku moja kaka alienda kwa mku wa mkoa kuomba msaada mwisho akakubariwa na akawa amechukulliwa akaishi kwake ila mimi sikupata kokote,
sikuchache baadae alikuja mtu mmoja kutoka kule Arusha akadai kuwa anahitaji wasichana wakwenda kule mjini kufanya kazi kwenye hoteli moja   kwa sababu sikuwa na kipato nikaamua niende angalau nipate chochote baada ya kwenda huko sikutegemea kumbe mtu yule alitafta wasichana wa kuuza mtu unauzwa ili yeye apate kipato yule alie kupeleka hakua mimi tu bari tulikuwa wengi wasichana tuliokuwa tunauzwa nilikuwa nauzwa ili watu watumie mwili wangu kwa starehe na ndipo ulipo nikuta najiuza kipindi kile nakumbuka na wewe ni moja wapo  wa watu nilio lala nao ila baadae nilipata ujauzito nikajifungua mtoto wa kiume nikamuita jina Esilomu ila kwakuwa sikuwa na uhakika na baba yake nikaamua kumpa jina la rafiki yangu aliekuwa anaitwa Ngwale, nilifanya hivyo kwa sababu baba yake kabisa nilikuwa simujui.
mambo mengi yalifanyika nikawa nataka kujiengua na kazi ile nakutaka kujifanyia kazi nyingine lakini yaliyo nikuta ndiyo yale uliyo yaona na hata hivyo nakushukuru kwa kuniokoa mpaka sasa niko hai ndiyo maana niko tayari kwa chochote kutoka kwako.
kwahiyo hayo ndiyo yaliyo nikuta mpaka sasa sijui wapi alipo kaka yangu na wala alipo mtoto wangu hata rafikiyangu Ngwale sijui kama ni wazima au laa!!
hiyo ndiyo historia yangu kiufupi." Penina alisema huku machozi yakimtoka, Gabri alishindwa kujizuia akamkumbatia nakusema "pole sana tena sana  sikujua yote hayo sasa mbona hukuniambia toka mwanzo mara tuu ulipo toka hosipitali?"

"muda wake ulikuwa bado sikutaka kukuchanganya wakati ule". penina alijibu.
"nikwambie kitu?" Gabri aliuliza
"ya! do it!!" penina alijibu
"Edisoni Mwasera bado anaishi"
"eti nini? kwani unamfahamu"penina aliuliza kwa mstuko mkubwa
"Ndiyo anaishi na habari njema ni kwamba nilipo chaguliwa kuwa raisi nilimteua kuwa jaji, nilimteua bila kujua kuwa yeye ni kaka yake na mtu nimpendae tena ninae mthamini, kwahiyo bado anaishi na nzuri zaidi mwanao Esilomu yupo hapahapa Dar na kwa kukufurahisha zaidi  kesho asubuhi angalia taarifa ya habari utajua nini kinaendelea lakini wote wapo hao watu mhimu kwako". Gabri alisema huku Penina akiwa anamuangalia kwa kushangaa kinacho tokea alihisi ni ndoto anayo kuwa anaota
"hapana Gabri acha kuniweka katika wakati mgumu namna hiyo" Penina alisema
"Penina trust me!" Gabri alisema
"siwezi kuamini gabri unacho niambia"penina alisisitiza.
"leo kaka yako amekuja nyumbani kwangu na kunisimulia kila kitu kilicho wapata na kama ulikuwa hujui alie waua hawa viongozi wawili yaani makamu wangu na waziri mkuu ni mtoto wako Esilomu".
"Nini?"
"Habari ndo hiyo, kwamba alie waua hawa watu wawili ni Esilomu Ngwale na kwa sasa yupo gerezani na alie toa hukumu ni kaka yako Edisoni alitoa hukumu bila kujua kuwa ni ndugu yake ila tuu elewa bado wapo tena wapo hapa hapa Dar, mimi nataka kuondoka kunasehemu naenda ila kumbuka Gabrieli wa leo siyo wa zamani mimi nilisha badilika sasa nitamsaidia Esilomu japo kuwa simujui baba yake" Gabri alisema huku akijianda kutoka mle chumbani
alisimama na kuanza kutembea kuuelekea karibu na mlango
"Gabri rudi kidogo.." Penina alisema.
alirudi na kusikiliza mambo ambayo anataka kuambiwa na penina.

"Gabri kama yupo Esilomu tafadhari nakuomba umpimishe vina saba vya damu yawezekana ni mtoto wako" Penina alisema
"unasemaje Penina?" Gabri aliuliza
"Ndiyo nimesema kwa kumaanisha.
pindi nilipo pata ujauzito hata wewe tulilala wote kwahiyo inawezekana Esilomu akawa mtoto wako"
Gabri hakuamini kabisa kusikia hivyo alimwambia penina
"penina nakupenda sana nakuthamini natena kama unavyo jua kuwa sina mtoto, siwezi kuamini nikija kujua kamba Esilomu ni mwanangu hakika siwezi amini haya yote lakini ngoja nikuache niende kushughulikia suara hili kwanza la Esilomu.
naenda ila pia nitapita kwa Edisoni ila sitamwambia chochote maana muda bado haujafika wa kuambiwa". Gabri alisema huku anainuka na kutaka kuondoka
aliinama na kumnong'oneza
"kama Esilomu ni mwanangu nakuahidi kufanya jambo laajabu ambalo watanzania watashangaa".
alimaliza na kuondoka
"haiwezekani eti Esilomu yupo? Edisoni yupo? Wako hapahapa dar es salaam? nitawapataje? ila ngoja nitaona kama ni kweri kuhusiana na swara hili."Penina alijiwaza huku akishika shavu lake la kuume kwa kutumia mkono wake wa kuume.
"Mungu wangu wewe mwenyewe unanijua Gabriel wa sasa si yule wa zamani mimi nilisha badilika sana ila kama huyu ni mwanangu nifunilie ili nijue hee kama ni yeye nitafanya sherehe kubwa sana sito amini kitakacho kuwa kimetokea ni ndoto nadhani hii ninayo iwazia haiwezekani Esilomu awe mwanangu nilitembea nae Penina siku moja haiwezekani mimi nikawa ndiye nilie mpa mimba lakini yote kwayote lazima nihakikishe kwanza kwa kupima vina saba vya damu ndipo nitajiamini ila kwa muda huu nielekee kwanza kwa jaji ili kumtaarifu kwamba sasa naelekea kutuma barua ya kutaka isitishwe zoezi la kumnyonga Esilomu mpaka pale ukweri utakapo patikana.
Gabrieli alikuwa akijiwaza huku gari linaelekea kwa jaji.
baada ya dakika chache alifika kwa jaji Edisoni
gari liliingia getini na jaji akashangaa kumuona raisi amekuja kwake haikuwa rahisi raisi kufika kwa mtu kama huyu na huku hana walinzi wake kama ilivyo zoeleka.
"aa karibu sana mkuu"jaji alisema akiwa anamkaribisha ndani
"asante sana" Gabri aliitikia akaingia ndani
"karibu sana"mke wake Edisoni Bi heleni alimkaribisha
"asante sana shemeji" Gabri alisema.
"unatumia nini? soda au?" Jesika aliuliza
"hapana wewe usilete chochote"
kabla hajamalizia mlinzi wa jaji Edisoni akaingia na kutoa taarifa kwamba
"mkuu kuna mgeni amekuja anahitaji kukuona vipi nimuruhusu aingie?" mlinzi aliuliza.
"ninani?" jaji aliuliza.
"amejitambulisha kuwa ni Dakitari Vijey Shaluma"  jaji alistuka sana yeye na mke wake wakaangaliana ,
"umesema Daktari Vijey Shaluma?" jaji aliuliza.
"ndiyo" mlinzi alijibu.
"mwambie asubiri nakuja" jaji akasema huku moyo ukimuenda mbio kwa kitu alicho ambiwa.
alimwangalia mkewe kisha akaangalia chini akasema kimoyomoyo "haiwezekani dakitari Vijey Shaluma amekuja huku tanzania? kwa nini? Vijey siwezi kukubari utoboe siri niliyo itunza sikunyungi zilizo pita haiwezekani" jaji alihisi maji mwilini baada ya kijasho chembamba kumtoka.


ITAENDELEA......
FUATILIA KISA HIKI CHA KUSISIMUA
LIKE AU SHARE AU COMMENT ILI TUWE WOTE PAMOJA.