BUSARA seaso ya 1, episode ya 7

Stori: BUSARA..part 1
episode ya...7
Mtunzi Ayubu Henry..

ilipoishia

mda mchache wakawa wameingia anga la pakistani na walitua huko sara akatoa amri kwamba asishuke hata mmoja mpaka atakapo sema.
aliogopa kuwasiliana na mau au chard kwa ulinzi wao, taarifa ilipo fika iliuliza kwani anataka nini?
akajibu anataka kulipiza kisasi cha baba yake marehemu mohammed.

taarifa zilimfikia mzee mwenyewe mohammed na uzuri alikuwako hukohuko pakistani.
Mohammed akatoa tamko kuwa anamhitaji huyo dada...................

ENDELEA...........

siku yote ilipita na ilipo fika usiku taarifa zilikuwa zimesambaa kila sehemu na hata hapa nchini na kila seacial media taarifa zilisambaa.

mda mchache tu kupita ilikuwa saa tano usiku raisi wa pakistani ndugu Shalifu Abduli alitoa tangazo kwenye ile ndege na kuuliza je, watekaji walitaka nini hasa kwa sababu mpaka sasa haijajulikana vizuri.

sara alijibu akisema anataka wamletee fuvu la marehemu baba yake na alipo jalibiwa kuhojiwa kuwa wao ni kikundi gani alijibu akisema mimi ni kundi moja na baba yake.

masa yalizidi kuyoyoma ikafika saa kumi alfajiri ikambidi sara ahofie kwa sababu ukizingatia moja hajui kama watakuja kumchukua au laa.

saa kumi na dakika kumi na tano yaani saa kumi na robo, mama mmoja akasema PNWDO  sara alishituka sana ila akajikaza mwisho akageuka na kumtazama yule mama, kidogo kidogo akiwa anamsogelea yule mama, naye yule mama akatenda jambo la ajabu akavua sura.
kumbe alivaa sura ya bandia ya kike na yeye siyo mwanamke ikaaminika hata sara hiyo siyo sura yake.

yule mtu akasema " toka nje helokopita inakusubiria acha hii kazi tumalizie" sara hakuongea kitu akatoka nje hakika kulikuwepo helokopita akaenda akapanda akaperekwa na ndege ikaachiwa, hakuna ugunduzi ulio fanywa wakuwafanya watu wawajue watu wale ni akinanani. ngege hii ilipita polini huo usiku mpaka sehemu ambayo ni ya sili sana kunapango kubwa na pango hilo wakaingia humo ndani na baada ya kuingia sara alishangaa sana kwa jinsi alivyo pokelewa kama malikia na kila mtu alimpigia magoti vyakula vililetwa akara huku akiwa kimya kuthibitisha yeye ni gaidi kama baba yake.

**************************************************

"Sasa mke wangu nilishakuwa kiongozi na uongozi wangu ni mkubwa sana ila wakati mwingine huwa nakaa na wasiwasi kuwa hawa watu ukiona tumeenda kinyume kwa jinsi wanavyo taka watatuua" Mheshimiwa waziri mkuu ndugu Ezii alikuwa akimwambia mke wake wake kipenzi.
"sawa kabisa nafrahi umelijua hili mapema na mimi kama mkeo nakushauri kuwa hao watu ni hatari ukiwa nao hakikisha unajiandaa kwerikweri usiwakosee sawa mme wangu?". mrs Ezii alishauri.

kimya kidogo kilipita kisha Ezii akasema mke wangu naomba kidogo nikuambie kitu ni kwamba sasa hivi hii siyo tanzania bali ni chakula cha marekani na kwa maana hiyo kila kitu sasa ni chakwao ila siyo tanzania tuu hata libia,kila mahari hapa afrika wanatawala.
harafu kesho wametuita tukutane kuna mambo tunatakiwa tuyajadili, kwa hiyo kesho tutaenda huko".**************************************************



kesho kufika
"Upande wangu sina shida na nadhani kuwa kunahaja ya kuweka mambo sawa kwa kuwalidhisha watanzania hasa tutakapo wagawia vyandarua dhidi ya malaria hakika watatuamini kwa hiyo wewe waziri wa miundo mbinu na wewe waziri wanishati nimewaweka kwenye kiti hicho kwa sababu nyie ni ndugu zangu na siwezi kuwasahau ila pia  wewe mkuu wa mkoa wa tabora wewe ni shemeji yangu ili nilazimu nikupe uongozi kwa hiyo nataka niwaambie kitu kimoja.

leo ilitakiwa tukutane na watu wanao tuongoza kuna mambo mengi ambayo walitaka kutueleza na naona watatuambia harafu nimesikia kuwa kuna jambo wanatarajia kulifanya ndani ya mwezi huu au ujao hawaja sema ila mimi kama raisi wa nchi hii napaswa kujua ni kitu gani.  ila msijali sana tutataarifiana kama watatuhitaji ila nawaomba msije mkaenda kinyume na hawa watu lasivyo tutaisha wote jalibuni nafasi zenu kisha mjue uwepo wenu  ni wa muhimu kwangu sawa?". raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania alisema na kumalizia kwa kusema "mkiona kuna mtu anaenda kuyafahamu haya yote sharti afe asitoe siri".

**********************

baada ya mda kupita edii alirudi nyumbani na kumweleza mke wake kisha akauliza "hee kwakweri sielewi busara alisha nichukia nikimpigia simu haipatikani na nina takribani miezi mitatu sionani nae sijui yuko wapi natamani aje kwangu na ukizingatia ni binti mzuri". alikatishwa na mke wake kwa kusema "sipendi umuongee huyo binti achana nae wewe jali yako".

Edii alisema "hiyo ni wivu au?"
"ndiyo sipendi"
"sawa kama haupendi sito rudia"

***********************************************************

Chard na Mauld walirudi tanzania moja kwa moja hadi Dodoma alipo Anita na Joel, walipokerewa kwa furaha kubwa lakini baada ya kufika nyumbani anita aliuliza "huyo ninani?"
Richard akajibu "huyu ni rafiki yangu na kuna mengi ambayo nitawaeleza lakini siyo sasa lakini kitu cha kufahamu huyu ni yule rafiki nilio waambia tutamwendea tukiwa na sara kama mnakumbuka?".
wote walijibu "ya tunakumbuka,!  karibu sana huku bara".

"asante"mau alisema.

kimya kidogo cha kama dakika mbili kupita Anita aliuliza "mbona tuliwatafta sana lakini hamkupatikana kwenye simu vipi kulikuwa na nini na sara yuko wapi?"

"sara hayupo humu nchini yuko mbalisana"chard alisema.
"wapi hapo?"anita aliuliza.

"yuko pakistani"chard alisema

"umesemaje?" joel aliuliza

"ndiyo yuko huko tutawasimlia yote tukitulia ila kwa sasa tuelekee zanzibar kwa ajiri ya ulizi wa sara kule kuna kila kitu".

***************************************************

Ridia feki yaani sara alisikia sauti ukimuita kwa upole sana akageuka akamuona bibi mmoja akisema "njo unifate huku chini".
walizidi kuingia ndani kabisa ya pango lile kitu cha ajabu hukohuko kuna maabara za kisasa na madokita ni wahali ya juu kunamambo mengi walikuwa wanafanya hasa kazi moja ya kutengeneza binadamu wenye nguvu sana.
kabla haja onana na Mohammed ikasemfekana lazima apimwe vina saba vya damu yaani DNA ili kuona kama ni mtoto wa mohammed, isije ikatokea wana mpeleka kwa mohammed kumbe wamepeleka nyoka,
kazi ikaanza akaingizwa chumba maalumu.........

ITAENDELEA

hakika kazi ipo je wakigundua siyo mtoto wake itakuwaje watamuua? au  itakuwaje? hakika sara umechagua kazi kubwa.
fatilia season hii ya kusisimua ina enda kwa jina la BUSARA season 1.
episode ya 7
ona zinazo fata bonyeza www.facebook.com/kingayuu