Stori: BUSARA..part 1
episode ya...8
Mtunzi Ayubu Henry..
ilipoishia
Ridia feki yaani sara alisikia sauti ukimuita kwa upole sana akageuka akamuona bibi mmoja akisema "njo unifate huku chini".
walizidi kuingia ndani kabisa ya pango lile kitu cha ajabu hukohuko kuna maabara za kisasa na madokita ni wahali ya juu kunamambo mengi walikuwa wanafanya hasa kazi moja ya kutengeneza binadamu wenye nguvu sana.
kabla haja onana na Mohammed ikasemfekana lazima apimwe vina saba vya damu yaani DNA ili kuona kama ni mtoto wa mohammed, isije ikatokea wana mpeleka kwa mohammed kumbe wamepeleka nyoka,
kazi ikaanza akaingizwa chumba maalumu.........
ENDELEA...............
baada ya mda ulipita sara yumo chumba cha madokita huku wakiwa wanataka kupima damu yake kuthibitisha kama ni mtoto wa Mohammed.
damu ilichukuliwa tayari kufanyiwa uchunguzi.
madakitari waliichukua damu ile na kuiweka kwenye vifaa maalumu baada ya dakika chache majibu yalitoka.
ilisikika sauti ya kushangilia, vipimo vya damu viko kama ilivyo tarajiwa hakika ana damu inayo fanana na baba yake. sara alijishangaa sana baada ya kuona damu ina fanana na Mohammed. kwanini ina fanana sara alijiuliza sana hakupatajibu akawa amehisi yawezekana madokita wamedanganya
"naamini hawa madokita wamedanganya ili waniokoe na kama wamenisaidia wanalengo gani na mimi? au wamesha nijua kuwa mimi ninarengo tofauti..... sijui itakuwaje natamani niwaambie akina mau na chard lakini naamini wamesharudi tanzania sasa nitafanya nini ila oke mimi ni mzuri ngoja nitatumia uzuri nilio nao kumfatilia kisha huyu baba yangu feki akijua kuwa moja kati ya wafanyakazi wake ananipenda atamuua ila kabla hajamuua inatakiwa anipe siri kwanini wameamua kumdanganya kuwa damu inafanana hii ni hatari kwao akija kugundua hili lililo tokea tutatamani dunia itoboke tuingie" sara alikuwa anajiwaza huku akipelekwa kwa yule alieshangilia
"karibu sana mwanangu kipenzi,
hahahahahahahahaha mtoto ana utundu kama baba yake". Mohammed alisema.
sara akasema "Acha kuigizia wewe bata baba yangu alisha kufa na alisha zikwa" kisha sara akaigiza kulia akasema "Toa hiyo sura unayo bambikiza eti ni baba yangu"
"Ridia, wewe haujui mimi ni baba yako na sijafa na hakika reo nifuraha kubwa sana"Mohammed alisema kwa furaha kubwa sana.
"kwa hiyo wewe ni baba kweri? na ilikuwaje waniambie kuwa ulikufa au ulifufuka? ninamaswari mengi ya kukuuliza ila nijibu hayo kwanza".sara alisema.
"mimi ni baba yako, wewe ni mwanangu na najua kuwa nina bahati kubwa sana kumpata mtoto kula unenepe hii ni dunia yako sasa".moha akawa amemalizia.
*****************************************
usiku ulipo fika sara alimtembelea dokita mmoja "dokita mchana nilipo kuona nilijihisi kuvutiwa nawe naomba ushirikiano wako"
dokita akasema "binti nakujua sana unaitwa Busara Hamisi na kama haujui ni kwamba wewe siyo mtoto wa Hamisi bari wewe ni mtoto wa Mohammed,".
sara alishituka sana baada ya kuambiwa hivyo alihisi kizunguzungu akauliza
"mbona sikuelewi we mtu kwanza wewe nani?".
"Binti mimi ni mtu nilie kula chumvi nyingi sasa kwa taarifa yako ni hivi wewe ni mtoto wa mohammed na ndo maana damu yako ilifanana sana na ya baba yako na pia wewe unatakiwa kujua kuwa unandugu yako mna fanana sana anaitwa Ridia,
hivyo wewe ni Rukia na mdogo wako anaitwa Ridia,
kwa sasa sina mda ila mtafte mtu mmoja anaitwa Dickison Maumba au CM yaani computer man anapatikana Braziri ukimpata atakusimulia vyote wewe ni nani? mnajuanaje na mohammed na Hamisi ni nani". sara ali dua mpaka kinywa kikawa kigumu kusema jambo hata kuuliza alishindwa.
dokita yule akasema "dada wewe ndo unaweza kuzuia hili linalo kuja ni zaidi ya sunami kwenye dunia ukilisikia zuia tafadhari na nakuomba ujalibu uisaidie dunia nakuamini mzuie baba yako asiletee hilo zuruba,
usiku mwema ila pia kumbuka ulizaliwa kuokoa dunia." dokita alimalizia akawa anaondoka.
sara hajawahi kuto sinzia ila usiku huo hakusinzia aliwaza sana yeye kwani ni nani? kwa nini mohammed ni baba yake na siyo Hamisi na je nizoluba gani linakuja kwenye dunia? hakika hakusinzia mwisho alijiuliza atampata wapi CM.??
********************
"basi tuambieni sara yuko wapi? sababu mlituambai tukifika huku zanzibar ndo mtatuambia tuelezeni" anita alisema kwa uchungu.
"Anita usiwe na wasiwasi iko hivi, kwanza sara ni mzima harafu simulizi iko hivi
tulipo fika huku mambo yalienda vizuri lakini kilicho tokea binti sara akasema anatafta kikundi cha mohammed ili ajiunge na madhumuni ni kwamba akikipata kikundi hiki; kwanza kinaitwa PNWDO,akisha kujiunga na hiki kikundi itakuwa rahisi kuwashika au kuwazuia".
"sawa ila haujasema yuko wapi!!"?,Joel alisema.
"yuko pakistani huko".
"jamani naona sara amesema kitu kwenye ile tovuti binafisi na alicho sema kinatisha hakika......njooni muone hehehehehehehehehehehe".
"kwani nini Mau" chard aliuliza.
njo uangalie kwenye komputer alicho kisema" mau alisema.
"mtuambie hata sisi" anita alisema.
"nafahamu mnajua kusoma njooni msome".mau alisema.
kila mmoja alitamani atoke kwenye dunia kwa kitu alicho wambia kinatisha...........................................
ITAENDELEA.......
sara amewatumia nini? au kasema ukwer kuhu yeye au kasema lipi ambalo wote marafiki zake wame choka?
fuatilia kisa hiki cha hatari kila siku ndani ya m.facebook.com/kingayuu
comment kama unaipenda season ya BUSARA 1, ndani ya facebook.com/kingayuu