HUKUMU YA HAKI sehemu ya 1

HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 1
HUKUMU YA HAKI
SEHEMU YA..1
Mtunzi Ayubu Henry

Nisiku ya tarehe 20 mwezi wa Aprili mwaka 2014 siku ambayo umma wa watanzania wakisubiri hukumu ya kijana mmoja  alie sadikika kuwa ndiye muuaji.
Jaji aliekuwa akisubiriwa mahakamani alifika na mara moja kesi ika funguliwa.
jaji ndugu Edison Mwasera akasema "kulingana na mashahidi wa upande wa walalamikaji yaani serikali na ushahidi ulio tolewa unafaa kabisa kutoa hukumu kwa kesi hii" akanyamanza kisha akaendelea " napenda kusema kulingana na mazingira ya tukio hili lilivyo fanyika na kukutwa kijana huyu na viashilia vyote vya kuashilia kuwa yeye ndo muuaji na hakuna hata shahidi kutoka upande wa mlalamikiwa,  kulingana na shelia ya mwaka 1990 kifungu cha 6 B natoa hukumu ya kifo kwa ndugu Esilomu Ngwale na mtuhumiwa anapewa siku tano za kuishi kuanzia sasa, kesi imekwisha" ikasikika sauti ikisema "koooooooooooooooooo"! kuashilia kesi imekwisha. Esilomu alichukuliwa mpaka jela tena akisubiri siku yake ya kunyongwa alionekana mwenye huzuni nyingi sana mpaka kesi inaisha hakuongea kitu ndugu huyu anae sadikika kafanya mauaji ya viongozi wakubwa kwenye serikali, yaani anashikiliwa kwa sababu kamuua waziri mkuu wa mambo ya ndani ndugu Ishimael Shemley  nakumuua ndugu Fabiano Andrew makamu wa raisi ya Jamuhuri ya muungano wa tanzania   inasadikika kawaua wote kwa siku mbili tofauti.
Ishimaeli alifaliki dunia mwa 2014 Januari ya tarehe 21 usiku na siku ya juma mosi kwa kupigwa risasi kichwani na Fabiano alifaliki siku iliyo fuata yaani tarehe 22 usiku siku ya juma pili kwa kupigwa na kitu chene incha kali kwenye paji la uso wake ambapo ndicho kilicho sababisha kufa kwake, wataaramu wanasema damu ilivujia ndani ikapelekea kufa kwake.



*
Siku moja kupita hukumu ilikwisha tolewa kwa kijana Esilomu na kusubiriwa siku ya kunyongwa kwake leo hii jaji Edison alikuwa nyumbani akijalibu kusoma vitabu vyake vya sheria mara akashituliwa na sauti ya mlango kufunguliwa, "my wife" jaji alisema "yes!!!" mrs Edson alisema, mama mwenye upole wa asiri na uzuri wa kiafrika ndugu Heleni Mwasera.
"mke wangu vipi mbona unaingia bila kubisha hodi hujui wenzio utatushitua? sijapenda" jaji alisisitiza
"nimekuelewa mme wangu ila sasa hata mimi najishangaa yaani toka jana utoe hukumu ya yule kijana sina amani kabisa mme wangu!" heleni alisema.
"hata mimi kwakweri sina amani naona kama hukumu niliyo toa kama inamakosa sababu nime hukumu kesi nyingi lakini hata jana niliota eti yule kijana analia kwa uchungu mkubwa alikuwa ananililia mimi yaani mpaka sasa sina amani kabisanajiuliza nashindwa kuelewa, ila pia mbali na hayo yote kunamaswari mengi najiuliza yule kijana toka kesi ianze sijawahi kuona wakili akimsaidia na wala hata shahidi sikuwahi kumuona na ukimuuliza je, aliua anakubari ukiuliza sababu anatoa machozi nakusema nilipenda kuua. kwakweri naona kuna umuhimu wa kumjua mtu huyu sina amani moyoni aliua kwanini na kama hana sababu wazazi wake wako wapi maana sijamuona hata mmoja pale kwenye kesi ile."

kweri kabisa mme wangu nadhani kunahaja ya kumjua mtu huyu na nafikili ili tupate amani lazima tumjue mtu huyu au wewe unaonaje  maana mimi naona damu hii haina hatia."heleni alisema
"ndiyo nimekuelewa na nadhani kesho kunahaja ya mimi kumfata huyu kijana kule jera ya taifa nikamuone". edison alisema.
"vizuri mme wangu ila pia kumbuka mwanao Jesca kesho anakuja siunajua leo usiku ndio ataanza safari kutoka Urusi kwenye mafunzo yake ya shelia?"
"duuu nilikuwa nimesahau kwahiyo anakuja kesho?"
"yes"
"oke wewe utaenda kumpokea airport ila mimi nitaenda kule jera sawa" edsoni akamuomba mkewe baada ya mda kupita jaji Edisoni aliendelea kujisomea vitabu vya sheria.


Nisiku ya tarehe 22 mwezi wa aprili mwaka 2014 jaji Edsoni aliamka asubuhina mapema na kwenda mazoezini kama kawaida yake alipo toka chumba cha mazoezi alipokelewa na harufu nzuri ya mlo wa asubuhi wa mkewe alio muandalia akajisemea moyoni "Nilioa hakika!"
mdamchache baadae alioga nakujianda bizuri mke wake alimfata na kumukaribisha chakula "my dear"mke akasema
"yes!! what problem do you have?" edd alisema kiutani kwani alijua nini mke kamuitia
mke akapiga goti la kiafrika kwa kumkaribisha mumewe kula chakula
mda mchache ulipita edison baada ya kujianda akamuaga mkewe tayari kwenda gerezani kukutana na mtuhumiwa wa mauaji ya vigogo wawili kwenye serikali ndugu Esilomu Ngwale
"my mimi naenda huko kukutana na huyu jama sijui atanipokeaje ila vyovyo vile najisikia kumsaidi kijana huyu japo nilitoa hukumu ya kifo nasikia damu yake inanililia."
"sawa mme wangu nadhani kuna haja ya wewe kufika huko ila mimi naenda kumpokea jesika nadhani ndege itafika saa 5 asubuhi, nakutakia safari njema mme wangu". heleni aliongea kwa uchungu kumwambia mmewe
"usijari sana ngoja nieleke huko   naomba funguo zangu za gari na pia naomba umwambie jesika asikalike kwakuwa sipo au sijaenda kumpokea"
Edison baada ya hayo akaingia ndani ya gari na kuondoka huku mke akitaka kujianda kwenda kumpokea mtoto wao aitwae jesca edson alikuwa Urusi kimasomo yanayo husu shelia.

**

Ni saa 4 na dakika22 kwa mjibu wa saa ya mkononi ya Edisoni, alifika pale gelezani ambapo sasa wengi wanapaita Jehanamu kwa sababu ya kujizolea sifa za kutowahi mfungwa yeyote kutoloka toka jera hili lianzishwe wakati wa ukoroni mnamo mwaka 1949 mpaka reo hajawahi kutoloka mtu yeyote.
"mimi naitwa jaji Edison Mwasera je, bwana jera nimemkuta?" Edson alijitambulisha kwa mpokea wageni "ndiyo yupo karibu jaji"
"asante"  jaji akajibu .
"nenda kule mbele kuna ofisi yake we bisha utafunguliwa mlango"
"nashukulu kwamsaada wako" edisoni aliondoka

"habari mheshimiwa jaji Edison" bwana jera aitwae Shabani Rashid.
"asante sana, vp za majukumu ndugu yangu"
salama tuu jaji vipi mbona mara nyingi huji hata kuniona ila leo vip imekuaje? ila tupo hahaha tupo sana."
"asante sana, ila leo nilikuwa nimekuja kumuona kijana mmoja".
"yupi tena?"
"huyu kijana alie hukumiwa kunyongwa na mimi mwenyewe ndiye nilie msomea hukumu."
"aaaaa oke ninamfahamu si huyu jama aneitwa Esilomu Ngware"
"yaaa ni huyo"
"sawa ila sijui kama ataongea na wewe jaji kwasababu toka mmlete hapa hii ni siku ya pili haongei chochote  hata nikiongea nae haongei chochote nikahisi atakuwa ameathirika na hukumu iliyo tolewa na sidhani kama ataweza kuongea na wewe, kweri sina uhakika labda ila sina uhakika" bwana jera alisema.

mda mchache ulipita kisha jaji akasema
"naweza kukutana nae unajua siyo rahisi mtu kuua watu wazito kama hawa harafu ukizingatia kuna mkanganyiko mkubwa ambao sielewi huyu kijana hana wazazi? na kama anao wako wapi? na mbona hawakuja kwenye kesi na kama kweri hana ndugu eeeeeeeeeee!  sijui anatoka wapi kwanini aliua?"
"nikweri jaji unapaswa kujiuliza lakini ngoja nikusaidie kukupeleka chumba alipo"
"sawa twende"
walienda selo namba P22RT alimo kijana Esilomu walikalibia huku moyo wa jaji ukienda mbio baada ya kukalia
"naamini ataongea nami maana sijaja kwa niambaya nimekuja kumuuliza kwa nini aliua na wazazi wake wako wapi sitakuwa na mengi .. .ila kweri atahitaji kunisikiliza wakati mimi ndiye nilie toa hukumu ya kunyongwa kwake, ila pia kwanini nimfatilie kama vile namjua simjui ila nadhani moyo wangu ndio ulio chagua". jaji Edsoni alikuwa anajiwaza mara wafika mlangoni wakaanza kufungua selo hiyo.
Esilomu alikuwa amejilaza japo likuwa haja sinzia machozi yalikuwa yakiendelea kutililika kama mvua ya masika akasikia mlango unafunguliwa wala hakugeuka aliendelea kujikunyata kama kuku mgonjwa   bwana jela aliingia mala mwenzake akaingia yaani jaji Edisoni.
"kweri anamatatizo mtu huyu"jaji aliwaza huku akimsogelea mfungwa mara Edsoni akaita "Esilomu?!!!!!"
Esilomu alishituka sana baada ya kusikia sauti ya jaji aliiongopa sana sauti hiyo akakimbia kimbia mle selo akitaka kujificha lakini asipapate pa kujificha.

Itaendelea .......
je,jaji ataweza kuongea nae au hapana na je kwanini Esilomu alichukua maamuzi mazito ya kuua kuna nini kinaendelea kuwa nasi sehemu ijayo
pata BONYEZA HAPA