HUKUMU YA HAKI sehemu ya 2

HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 2

HUKUMU YA HAKI
SEHEMU YA..2
Mtunzi Ayubu Henry

ilipo ishia

Esilomu alikuwa amejilaza japo likuwa haja sinzia machozi yalikuwa yakiendelea kutililika kama mvua ya masika akasikia mlango unafunguliwa wala hakugeuka aliendelea kujikunyata kama kuku mgonjwa   bwana jela aliingia mala mwenzake akaingia yaani jaji Edisoni.
"kweri anamatatizo mtu huyu"jaji aliwaza huku akimsogelea mfungwa mara Edsoni akaita "Esilomu?!!!!!"
Esilomu alishituka sana baada ya kusikia sauti ya jaji aliiongopa sana sauti hiyo akakimbia kimbia mle selo akitaka kujificha lakini asipapate pa kujificha.

ENDELEA..

saa tano ilitimia ndege ikafika tanzania
"waooooooooooooo" mama jeska yaani Heleni alimkalibisha mtoto wake
"mama nime kukumbuka"jesika alidai
"hata mimi mwanangu, umenawili hakika kidogo uwe murusi" wote wakacheka
"hapana mama  mimi ni mwafrika mzuri na siwezi nikawa murusi, eheeee nimekumbuka baba Jesika nae yuko wapi mbona simuoni" jesika alidai
"yupo lakini siunajua kazi ya baba yako? hakai leo kunasehemu kaenda ila nadhani tunaweza mkuta au hatakama hatuta mkuta atakuja tuu yeye mwenye amekukumbuka" mama alisema akiwa anachukua mzigo yaani mabegi na kuelekea garini tayari kuanza safari. wakiwa ndani ya gari Jesika akasema "mama tanzania imebadilika sana toka niondoke miaka minne iliyo pita sikutegemea kuwa tanzania imebadilika namna hiyo ila vizuri sana"
"Jesika unajua hizi inchi zinazo endelea ni haraka kubadilika kama ukitoka ukiludi unakuta pamebadilika sana"Heleni alimwambia mwanae 


Baada ya mda wakafika nyumbani "jama mda mrefu nimepakumbuka sana nyumbani sikutegemea kufika haraka hivi, hakika nyumbani ni nyumbani" jesika alisema.
akaendelea "mama kwahiyo baba aliunda wapi?"
"baba yako kaenda jela kuna mtu kaenda kumuona"
"nani mama?"
"kunamtu flani kaenda kumuona nadhani mda bado nitakuambia"
"sawa mama"
.


"sasa kaoge mimi nakuandalia chakula" mama akasema
"hapana mama mimi ni msichana eti unipikie acha nikajipikie" jesika alidakia
"wewewewe wewe ni mgeni kaoge heeeeee" mama alisema wote wakaangua kicheko ila Jesika akaenda kuoga.





."Esilomu naomba kidogo unisikilize, nahitaji kuongea na wewe na nakuomba sana"jaji Edisoni alimuomba Esilomu.
"jaji naomba mimi nikuache hapo"bwana jela alisema.
"sawa ndugu yangu" jaji aliitikia.

mdamchache ulipita edison akasema " Esilomu najua mtu anaweza kutenda kosa lakini kwa nini usinipe mda wa kuongea nawe? tafadhari nakuomba nipe wakati niongee na wewe".
"unataka nini kutoka kwangu au unataka unipunguzie siku, fanya hivyo ukitaka ila kama ni kuhusu mimi kama niliua kweri niliua nilimuua makamu wa raisi na waziri wa mambo ya ndani unataka lingine niache niache niache niache" Esilomu alisema huku akitokwa na machozi.
"naelewa uchungu  ulio nao lakini napenda nikuambie hivi  niko tayari kukusaidia naomba uniambie machache nitakayo kuuliza". jaji alisema.
"kwani unataka nini kama ni hukumu siulisha hukumu lingine lipi?" Esilomu akadai
"ndiyo naelewa yote lakini tafadhari nakuomba unisikilize tafadhari nakuomba" jaji akasema huku akimubembeleza.
"kwani nini unataka?"
"nataka nikuulize je unaweza ukanipa nafasi?"
"sikia jaji mimi ni muaji niliua kwani kunajambo lingine la kuniuliza au?" Esi alipata ujasili akasema kwa sauti kidogo.
"Esi naomba kwanza nikutoe wasi wasi sijaja hapa kwa ubaya nimekuja hapa kwa uzuri, labda nisikufiche toka hukumu niitoe sina amani kabisa na hata hivyo nadhani hukumu ilitolewa baada ya ushahidi kudhihilisha kuwa unakosa na una hatia
japo hayoyote ila swari ninalo jiuliza nije wewe ninani? ndugu zako wako wapi? na kidogo historia ya maisha yako na ikiwezekana uniambie kwanini uliua tena watu wakubwa kwenye selikali!!  
tafadhari nakuomba unge nieleza ili nijue nakuahidi kukusaidia japo kuwa zimebaki siku tatu wewe unyongwe lakini naahidi kukusaidia"  alimalizia jaji kwa kusema "tafadhari niamini!"

kimya kilipita kisha Esilomu akasema "sijawahi kukutana na mtu yeyote wakusema atanisaidia nikiwa na wakati mgumu kama huu ila reo nashangaa sana, jaji mimi nimuuaji".
"Esi naelewa lakini"
"hakuna cha lakini mimi ni muuaji wewe ni jaji hata nikikuambia huwezi kunisikiliza mwisho utabaki na kushangaa na kuumia bure na hata nikikuambia historia yangu haina umuhimu!!"
"Esi inaumuhimu sana tena sana nataka kukusaidia kwanza lazima nijue kwa nini uliua na kwanini ndugu zako hawakuja kwenye kesi!! kwa sasa wako wapi ndugu zako?"

Esilomu akamuangalia jaji kwa umakini akasema "jaji sipendi mtu yeyote aijue simulizi yangu".
"kwanini?".
"kwasababu ni mbaya sana"Esilomu akajibu.
"naomba uniambie"
mda mchache ulipita kisha Esilomu akasema.
"Wengi wananiita Esilomu Ngwale,    Ngwale siyo baba yangu bali ni mtu alie nilea sikubahatika kumjua baba wala mama ila Ngwale aliniambia kuwa alikuwa rafiki yake na mama yangu na mwishoni mwa mwaka 1989
mama yangu akafariki na baada ya kufariki nikachukuliwa na rafiki yake yaani huyo mwanaume anae itwa Ngwale anasema alinichukua kutoka kwa mama nikiwa na umri mdogo sana  yaani mwaka mmoja na baadae akanilea na mimi nimekuwa nadhani yeye ni baba," alinyamanza kidogo na kuomba apewe maji ya kunywa  uzuri jaji anapenda kutembea na maji safi ya kunywa kutoka kwenye kampuni moja maarufu sana hapa nchini.
"chukua haya hapa"
akachukua na kunywa kisha akaendelea na simulizi yake.
"Ndani ya miaka yangu sita sikujua biashara aliyo kuwa anafanya baba huyu yaani Ngwale ila tuu nilimuona ana maisha mazuri, nilipo timiza umri wa miaka nane nikahitaji kumjua mama yangu, hii ilikuwa mwaka 1996 nilimuuliza baba lakini alicho niambia mama alisha faliki, nilihitaji kumjua lakini sikufanikiwa, nakumbuka ilikuwa mwezi wa desemba mwaka huhu 1996 usiku jama mmoja alikuja pale nyumbani na kumufokea baba sikujua kwanini anamfokea na kumtukana  kwa jinsi navyo mjua baba alivyo mkari angeweza kumpiga lakini alimheshimu sana tena".  Esilomu alikatishwa na kengele iliyo lia pale magereza kuashilia chakula tayari wafungwa wote wanao hukumiwa kunyongwa na wa kifungo cha maisha wakapate chakula.
jaji akapiga simu "Hallo"
"halloo!" sauti ilisikika ya upande wa pili.
"ndugu yangu nakuomba umuagizie huyu mfungwa chakula kizuri kimfate hukuhuku".
"sawa jaji chakula kinaletwa" huyo mtu alijibu.

Baada ya muda chakula kililetwa na baadae chakula kwanza kabla hajakila  akauliza kwanini unanifanyia hivi
"sijui kwanini ila mungu tu na hata hivyo najisikia moyoni kufanya hivyo"jaji alisema huku akisubiri Essi amalize kula.

Muda mchache kupita Essi alishamaliza kula tayari kuendelea na simulizi.
"baada ya kuona baba ameingiwa na hofu nikashituka sana na yule mtu akasema sito kuajiri tena
alimaliza na kuondoka  nikaona nimuulize baba kinacho msibu, ilipo fika usiku nikaamua kumuhoji lakini alicho niambia sikuamini, alisema 'mimi siyo babayako mzazi na kamahaujui ni kwamba mama yako alikuwa anafanya kazi kwenye Nyumba moja ya wageni hapa hapa Arusha na nimarufu sana imejizolea sifa kubwa kwa kutoa huduma nzuri na inaitwa Yellow Geast house alikuwa anafanya kazi pale na kazi aliyo kuwa anaifanya ni kuuza mwili wake ametumiwa na watu wa kila aina kwa siku alikuwa akipata 10000 au hata kidogo hii ilitokana nakwamba kila biashara aliyo kuwa akiifanya ilimlazimu kukusanya kwa bosi na bosi ni mtu mkubwa sana kwenye nchi hii, na baadae mama yako akapatwa na maradhi yaliyo musumbua sana na mbaya alipata mimba yako mwisho akakuza na wewe kingali bado siyo mzima akawa anafanya biashara ile ya kuuza mwili wake ilipofika mwezi wa Novemba mama yako akahitaji akahitaji kujiuzuru kazi hii laki yule bosi kwakuwa alikuwa ni mtu mkubwa kwenye selikali akaamua kumuua mama yako kwa kumpiga risasi kichwani akawa amekufa na mwisho nikaamua nikuchukue ila hata hivyo mimi unahaja ya kujua stori yangu?' nilikubari japo kichwa kilikuwa kimechoka sana kwa maneno niliyo ambiwa akasema 'mimi nikwambie ninafanya kazi kwenye Hoteli moja hapa Arusha na kazi yangu ni ushoga' kwakweri jaji nisikudanganye baba alipo tamka ushoga alilia na kusema 'mimi mwanangu ni shoga na nilianza kazi hii mda mrefu na hata hivyo huyo mtu uliemuona akinifokea ni tajili alie niajili na mala nyingi natumiwa na kiongozi mmoja wa serikali kwa hiyo mwanangu kula lakini mimi ni shoga na mama yako alikuwa ni kahaba'
baba alimaliza na kuniacha pale sebleni nikishanga nikiwa naona yote ni ndoto."

jaji alijihisi kulia machozi yakimlenga lenga na baadae jaji aka jikaza na kusema
"pole sana Essi kwa taabu hiyo na vipi ilikuwaje ukaja dar na kwanini hawa watu uliwauwa na kama utaweza je huyu mzee Ngwale bado yupo".
Essi akajibu "Ngwale alishakufa"
"haaaa pole sana na kwanini alikufa".
"sababu kubwa ipo ila siijui ila ila hata hivyo kifo chake ni chakusikitisha alipigwa na kitu cha ncha kali kichani kwenye paji la uso" essi alisema.

jaji akauliza "je, unamjua mamayako anaitwa nani yaani aliitwa nani? na kwanini huyo baba yako mlezi alikufa, na kwa nini hawa viongozi uliwaua?.



ITAENDELEA..

BONYEZA HAPA