HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 3

HUKUMU YA HAKI 3 HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA..3 Mtunzi Ayubu Henry ilipo ishia jaji alijihisi kulia machozi yakimlenga lenga na baadae jaji aka jikaza na kusema "pole sana Essi kwa taabu hiyo na vipi ilikuwaje ukaja dar na kwanini hawa watu uliwauwa na kama utaweza je huyu mzee Ngwale bado yupo". Essi akajibu "Ngwale alishakufa" "haaaa pole sana na kwanini alikufa". "sababu kubwa ipo ila siijui ila ila hata hivyo kifo chake ni chakusikitisha alipigwa na kitu cha ncha kali kichani kwenye paji la uso" essi alisema. jaji akauliza "je, unamjua mamayako anaitwa nani yaani aliitwa nani? na kwanini huyo baba yako mlezi alikufa, na kwa nini hawa viongozi uliwaua?. ENDELEA... Muda mchache kupita kupita jaji akapigiwa simu huku akimusubiri Esilomu kuendelea na stori yake "halooo!!!" jaji alisema. "haloo baba shikamo" Jesika alimpigia baba yake simu, "aaa Jesika habari mwanangu? umesha fika?" "ndiyo baba ila mimi baba sijapenda" "kwa nini mwanangu?" "kwa sababu hujanipokea!!!!" "aaaa mama usiumie kunajambo nalifanya huku nilamuhimu ila mda mchache naweza kutoka nikaja nisubiri mwanangu sawa!!?" "ayaaa baba kazi njema ila nilikuwa na shida". "shida gani mwanangu?" "ukija uniletee pipi!!!" "hahahahaha ayaa mwanangu" jaji akacheka na kukata simu "Naomba basi uendelee na historia yako na umalizie nikitu gani kilicho muua baba yako mlezi na kama unawajua walio muua basi uniambie na kwa kumalizia uniambie kwa nini uliua na kwanini upo dar tafadhari naomba unisimulie, Esilomu hadithi yako inaumiza ila ili nikusaidie lazima nikujue tena kama una mjua mama yako jina basi unaweza kuniambia" Esilomu alimwangalia jaji usoni harafu akaangalia chini kisha akaendelea. " Kwamjibu wa rafiki yake na baba yaani jama mmoja aitwae Efurahimu John aliniambia kuwa kifo cha baba kilikuwa hivi cha utata sana na hakujua kilicho fanya apoteze maisha ila tuu alinipa historia ndogo kuwa 'baba yako mzee Ngwale alikuwa ni rafiki yangu na kabla hajafa aliwahi kuniambia kuwa wewe hata akifa basi nikutunze nilijaribu kuhoji sababu ya kusema hivyo lakini nilikosa mwisho akakutwa amekufa na sehemu aliyo fia ilikuwa ngumu kupata ushahidi na watu wakafikiri kuwa baba yako amejiua baada ya siri zake kuwa yeye ni shoga na hakuna mtu alie jua ukweli lakini baada ya mazishi ya baba yako nilienda nyumbani nikijiuliza kwanini kajiua ila je kama kajiua mbona kana kwamba kapigwa na kitu chenye ncha kali kichwani hii ikanijengea picha kuwa aliuawa kwa kuuliwa nilijitahidi kufanya uchunguzi mkubwa lakini sikufanikiwa kujua mwanzo wa kifo chake ndugu yangu huyu yaa Ngwale ila kijana wangu ukikua jalibu kufatilia kilicho muua baba yako ila pakuanzia nakuomba uanzie sehemu aliyo kuwa akifanyia kazi' sasa ndugu jaji hayo ndiyo aliyo niambia jama huyo alie kuwa karibu sana na baba ila mwisho baadae nilikosa msaada nikakosa pakuenda!!" jaji akauliza "ndipo ukaja dar baada ya kukosa msaada? au uliishi kwa huyo Efulahim?" "hapana sikuishi kwake ila tuu nilicho amua niliamua kujiunga na kikundi cha kuuza madawa ya kulevya na kwakuwa nilikuwa mtu nilie jituma hakika kikundi kile wakanilea mpaka nikakua ila kazi zetu ilikuwa ni kusafirisha madawa kutoka humu nchini mpaka nchi nyingine na kwakuwa kule Arusha kunamashamba ya bangi na kunapokea aina zote za madawa ya kulevya sisi watoto tulikuwa tunasafirisha madawa kutoka arusha na kupeleka sehemu nyingine na kibaya zaidi muda wote tulio kuwa tunafanya kazi nikama miaka mitano ila mbali na kuwa ilikuwa miaka mitano nafanya kazi pale ila niliambiwa tunamfanyia kazi mtu mmoja tajiri lakini sikumjua, muda mwingi ulipita baadae siku moja nilipewa kazi ya kupeleka dawa za kulevya sehemu moja penye ulinzi mkari ila nimepewa mimi hiyo kazi na nikaahidiwa kuwa nikiweza kufikisha hayo madawa nitapewa nyumba nzuri na kiasi cha pesa ila lazima nifikishe huo mzigo". jaji akauliza "sasa ikawaje?" "Baada ya muda madawa yale nikapewa na baada ya kupewa nikapeleka huko nilipo ambiwa nipeleke na njiani nilikutana na matatizo mengi kiasi kwamba nilijutia ila nikawa najipa matumaini sikuwa na sehemu ya kulala wala sehemu ya kuishi ndiyo maana niliamua kufanya hiyo kazi baada ya kupeleka nilifikisha yanapo hitajika kwenda basi nikarudi nyumbani hapo ndipo nilipo mjua bosi na kwa bahati nikajua ni yule yule alie kuwa akimtumia baba na ndiye alie kuwa bosi wake yaani bosi wa baba yangu nilifatilia malipo nikakosa mwisho niliambiwa nitakuja kuuwawa sasa niliumia pindi alipo niambia ataniua kama alivyo muua baba, hakika niliumia sana sana tena sana nilicho amua ni kulipiza lazima nilipize" Esilomu alisema huku macho yakilengwalengwa na machozi jaji akauliza "kwani aliitwa nani huyo bosi na je ulilipiza?" "huyo bosi wakati ule alikuwa raia tuu lakini baadae akawa amejiingiza kwenye mambo ya kisiasa na hatari akawa amechaguliwa akaja huku dar na kibaya zaidi akawa bado anaendelea na biashara mbaya za madawa ya kulevya amefanya hiyo kazi akiwa anacheo kwenye serikali alie kuwa anaijua ni mimi kazi anayo ifanya nikaamua kuja dar kumfuata ili nimufikishe mahakamani lakini nilipo jalibu kufanya mkakati wa kufikisha ushahidi polisi haohao polisi walinigeuka nikaamua nimuue kweri nilifanikiwa kumuua" jaji akauliza "aliitwa nani?" kimya kidogo kilipita Esilomu akasema " ni huyu kiongozi wenu Fabiano Andrew". " Fabiano Andrew?" jaji aliuliza "ndiyo" "huyu kiongozi?". "ndiyo?" jaji alihisi kuchanganikiwa kwa mambo aliyo ambiwa alitamani kujua na huyu mwenzake ilikuwaje kwasababu aliua watu wawili ndugu Fabiano Andrew na Ishimael Shemley ambae alikuwa waziri mkuu wa mambo ya ndani . Muda mchache ulipita akiwa jaji mala akasema "pole sana kijana wangu kwa yote hayo ila bado natamani kuendelea na habari hii ila usijali kesho nitarudi huku kukuona ili tuendelee usijali nitakusaidia wewe niamini sawa Essi?" essi aliitikia mala jaji wakaagana akaenda mana jioni pamesha anza kuingia alipita kwa bwana jera wakaagana na kuondoka kwa ahadi kwamba kesho atarudi. Saa kumi na moja jioni tulivu jaji alikuwa akijiwaza sana jinsi ya kumusaidia kijana yule muuaji alie ua aliwaza sana na kuufanya mwili wake unyongonyee akafika nyumba mulizi alifungua mulango akawa ameingiza ndani gari na kupaki pembeni kidogo karibu na gari ya mke wake alipo iweka "waooooooooo baba!"jeska alisema "waoooo baby" "baa nilikungojea sana" "hata mimi jesika nimeku kukumbuka sana na vipi maisha ya huku uzunguni" "nimazuri lakini hayawezi kuzidi ya nyumbani, nyumbani ni nyumbani bwana kule simuoni mama wa baba naonana na wazungu tuu" "karibu tanzania...." hajamalizia mama jesca Bi heleni akadakia "nimesha mkaribisha bwana wenae na mwanao heeee" "baba kwanza umeniletea pipi?" jesika aliuliza baba ajajibu "ndiyo kwanini nisikuletee" akampa pipi moja zilikuwa tatu na baba akachukua moja na nyungine wajampa mama "hahahahaha baba ndomaana nasema nyumbani ni nyumbani siyo kwamba siwezi kununua pipi lahasha ila itokayo kwa baba ina vitu zaidi ya pipi" jesika alisema huku wote meno nje wakiwa wanacheka. waliingiandani mala baada ya chakula cha usiku walikaa wakiwa wanabadilishana mawazo. Muda mchache kupita Heleni akamuuliza mmeo " Eddi vipi ulionana na yule mfungwa na kama mlionana alisema nini?" Eddi aliguswa kwenye kidonda kilicho kuwa kimepoa "nilionana nae" "vipi ni yeye kweri aliua au? kwani yeye alisemaje" heleni aliuliza. "mama jesika yule kijana ni muaji lakini kuna sababu iliyo mpelekea kuua na sidhani kama nitapata njia ya kumsaidia" "kwani alisemaje"heleni aliuliza "mimi nilimuuliza maisha yake yako nilidhani nimafupi kumbe marefu sana na pale alipo hana wazazi na hamjui baba yake nawala hata mama yake mwenyewe hakuwahi kumwambia mwanae kuwa baba yake ninani maana alikufa kingali Essi ana umri wa mwaka mmoja ilikuwa mwaka 1989 ndipo mama yake alipo faliki kuhusu jina la mama yake hajaniambia lakini alisematena kwamba mama yake alikuwa ni kahaba alipo kufa alichukuliwa na mzee mmoja anajulikana kwa jina la Ngwale alimulea ila pia yule mzee alikufa kwa mazingira ya kutatanisha na historia yake huyo mzee nikwamba alikuwa ni shoga" Heleni na Jesika walishituka sana washawishika kumjua zaidi huyo Esilomu aliwaeleza yote na ahadi ya yeye kukutana tena kesho aendelee kusimulia historia yake na kwa nini aliua, Jesika akasema "baba naomba na mimi kesho twende wote nikamuone je ukotayari" mzee akafikiri kisha akatoa jibu kuwa kesho wataenda wote wawili. ITAENDELEA TUKUTANE SEHEMU IJAYO.. MPENZI MSOMAJI LIKE NA COMMENT CHOCHOTE ILI NIJUE KAMA TUKO PAMOJA NAWATAKIA AFYA NJEMA.