KIDNEY SIMULIZI......................KIDNEY MTUNZI.........Ayubu HD MAWASILIANO......+255746207667 Email:..Ayubuhenry25@gmail.com
☆
☆
☆
☆
☆
Mnamo saa mbili usiku binti Veronica Jumbe alikuwa akilisogelea gari lililokuwa mbele ya nyumba moja iliyokuwa na mwanga hafifu huku akitembea kwa kunyata ili asionekane, kutokana na mwanga hafifu wa eneo hili la kificho hakuonekana na mtu yeyote. Alizidi kulinyatia gari hili na akiwa anaangaza kila pande ili kama kuna mtu yeyote ambae anamuona "Nimejitolea kwa chochote ili mradi niwe na wewe najua umeteseka sana kunipata ila huwezi amini hata mimi nimeteseka sana kukupata, sijui nikuambie jambo gani ili unielewe ila naona sawa na kipofu aliekuwa jagwani na amepata bahati ya kupata mwokozi hakika ninafuraha kubwa moyoni kuwa na wewe, wakati mwingine natamani ningekuwa mafuta unayo jipaka ili wakati wote nikutie harufu nzuri ili wenye wivu wakome." sauti ya mwanaume ilisikika ndani ya gari huku Veronica akizidi kulisogelea na kua makini na kusikiliza kilicho kuwa kinaongelewa na watu waliokuwemo ndani ya gari hilo la kifahari. "Kenedi huu ni usiku na kama unakumbuka nyumbani sikuaga naomba unirudishe kwanza tutaongea kesho mchana nakuomba sana, baba atanitafta atakapo toka gengeni kila akija lazima anitafte na ukizingatia mimi nategemewa pale nyumbani, naomba sana" sauti ya kike ilisika ndani ya gari hili, Veronica baada ya kulisogelea gari hilo kabla hajajua ni nani nani wamo ndani ya gari, gari liliwashwa na kuondoka. bila kupoteza mda Veronica alikimbia kwa kasi na kuingia ndani ya gari alilokuwa amelisimamisha pembeni kidogo ya kinjia, aliwasha gali na kuikimbiza kwa kasi kulifuata gali lile alilokuwa na wasiwasi. kwa mwendo aliokuwa nao ilimchukua dakika chache kulifikia gali lile, moyo ulikuwa unamuenda kasi na kupata shauku la kujua kunanini kinaendelea, bila kupoteza hata dakika alikuwa nalo sambamba huku akichungulia ndani kutaka kujua kuna nani, kutokana na vio vya milango kufungwa ilikuwa ngumu kufanya utafiti huu au kugundua chochote kutokana na vio kuwa vya rangi nyeusi. kadiri dakika zilivyo zidikusonga mbele Veronika alikuwa anahisi kizungu zungu "Eeee Mungu naomba hari isijirudie tena" Veronika alikuwa akijiongelesha huku akimuomba Mungu. Mda wa dakika chache Veronica alishindwa kulifatilia kutokana na kuzidiwa na hari iliyo mkuta. alichukua simu na kumpigia rafiki yake kipenzi Maua "helloo veronica" sauti ilisikika "Maua hari imerudia tena na hapa natapatapa nahisi kizungu zungu sana naomba unifate sitaweza kufika nyumbani tafadhari naomba unisaidie" Veronica alisema "Pole Vero kwani uko wapi? jamani?" Maua aliuliza "njiani natokea njia ya huku mjini naomba unifate tafadhari" alisema na kukata simu "hello!? hello!?" Alibaki akiita lakini Veronica alikuwa kakata simu.
★
★
★
kwenye nyumba ya kifahari iliyo pambika kwa bustani za kupendeza na maua yanayo tia harufu ya marashi, "Vero? Vero amka basi" Sauti ya Maua kumuasha Veronica ilisikika dakika chache Vero aliamka "Kuna nini?"Vero aliuliza "mmh vipi vero umechanganikiwa au"Maua aliuliza "Kenedi yuko wapi?" Veronica aliuliza "wee vipi unaongea nini mbona sikuelewi? Kenedi yuko nyumbani kwake"Maua alijibu "Hapana hayupo nimemshuhudia yuko na mwanamke mwingine,!" Veronika alisema "Embu pumzika naona una kichaa wewe, Kenedi yuko nyumbani jamani". Maua alidai "Nakuambia hivi sina kichaa niko sawa ila nimemshudia kabisa." Veronika alisema "aya umemshuhudia wapi? na akiwa na nani?" Maua aliuliza "Nilikuwa nimetoka kwa dr Andason kwa bahati nikaona gari la Kenedi imesimamishwa pembeni kidogo ya nyumba ila karibu pia na njia, nikaamua kusimamisha gari langu na kuisogelea gari lile nikawasikia wakiongea ila sikubahatika kulifikia sababu nilipo karibia gari liliwashwa na kuondoka, sasa sijui kwa nini Kenedi kaamua kuniumiza kiasi hiki." Veronica alidai "Hapana vero usiwaze sababu kwanza huna uhakika wa jambo hili na katika maisha kuchukua uamzi wowote bila kuwa na uhakika ni makosa" Maua alisema "Maua siwezi kuelewa kabisa sababu kama..... jamani kwanini lakini afanye hivi wakati" Veronika alikosa pumzi akashindwa kuongea "Vero mbona unajitabisha kiasi hicho kwa kitu usichokua na uhakika wa jambo? embu angalia hari yako na ujaribu kupima ni kiasi gani unavyo jitaabisha embu jizuie jamani". Maua alisema huku akimshika mkono rafiki yake Veronika "Maua unajua mapenzi yanaumiza mbali na jinsi navyo umwa ila hawezi akanikosea kiasi hiki, anafahamu fika kuwa nampenda asinge nifanyia hivi jamani, Maua?" Veronica aliita "bee!!!" Maua aliitikia "Naomba nikalale kwanza sijisikii vizuri!" Veronika alisema "sawa, vipi hautakula sababu chakula tayari!?" Maua aliuliza "Usijari Maua asante lakini, hapa sijisikii kula chochote naomba nikalale tu!" Veronika alisema huku akisimama na kutembea kuelekea chumba chake kulala. Usiku mzima hakupata usingizi na alikuwa analia huku akiiangalia picha ya Kenedi iliyokuwa kwenye meza ndogo iliyokuwemo chumbani mwake. "Kenedi nakupenda na ndio sababu nikajitolea kufa kwa ajiri yako na sikutamani hata kidogo uumie wala ukwazike kisa mwili wangu wala maisha yangu, nilikukabidhi kila kitu ili mradi uwe na mimi na usiniache, sijui na siamini nilichosikia nahisi ni ndoto" Veronica alikua akiwaza huku anatoa sauti ya maneno. ★ ★ ★ ★ Saa tano na dakika kumi na moja kwa mjibu wa saa ya mkononi mwa Kenedi, "Haloo ?!" Kenedi aliitikia baada ya kupokea simu. "samahani Kenedi vipi unaweza kunisaidia mpenzi wangu? ila samahani!!" sauti ya upande wa pili ilisikika "Seda jamani embu kuwa huru mimi ni wako na kwa tatizo lolote niko radhi kukusaidia" Kenedi alisema "Asante sana Kenedi ila nisaidie kweri utaweza?" Seda binti anae pendwa na Kenedi alisema "sema jamani usiogope" Kenedi alisema "Kenedi naogopa kufa, namuogopa Veronica naomba umwache ili uishi na mimi tu. pia nisaidie milioni mbili tafadhari" Seda alisema "Seda, kwanza nikutoe wasiwasi Veronica mimi nimesha mwacha ila hajui tu acha pia hata hii pesa atoe yeye ili nikupe wewe. huwa namuangalia nashindwa kumuelewa mwili mwembamba kama kama kuni za masikini au mwiko wa kusongea ugari harafu eti awe na mimi si ujinga huo acha bwana hanijui, unajua hanijui mimi naitwa Kenedi mtoto nilie kulia shida hivyo hawezi nitisha" Kenedi alisema na kumfanya Seda afrahi na kushinda kujizuia akasema "siyo kila mwanamke wa tanga anajua mapenzi wengine ni uchafu kwa waume zao kila siku lawama zisizo isha". Seda alisema na kuzua uchambuzi wa kumchambua Veronica. Walimchambua Veronica na mwisho Seda alikata simu na Kenedi akaendelea na kazi zake nyumbani kwake. Dakika tano kupita simu iliita "Huyu anataka kuniambia nini?"Kenedi alijisemea moyoni huku anataka kupokea simu ile,***********
*
*
*
*
Usikose ijayo, fuatilia kisa hiki cha kusisimua like na comment ili tuwe pamoja. kidney ni simulizi iliyo beba ukweri wa baadhi ya watu, ni kisa ambacho sijui wewe unge fanya nini ukiwa mshiriki wa hayo au kama mapenzi yamesha kuumiza ulifanya ninu? fuatilia ujue kilicho tokea kwa wenzetu, Kenedi,Veronica,Seda na wengine wengi tu.
KING AYUU
kidney
HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 7
HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 7
HUKUMU YA HAKI
SEHEMU YA..7
Mtunzi Ayubu Henry
ILIPOISHIA....
Haiwezekani eti Penina Mwasera ana mtoto tena ni mtu alie saidia kuiokoa tanzania he! mbona sikulijua hili mapema ngoja nifatilie kwanza sababu haiwezekani". raisi alikuwa anajiwaza huku akieleka sehemu ambapo magari yana pakiwa na kufunguliwa mlango akamwambia mwendesha gari
"naomba twende Nyumba namba H2029 balabala namba 32 fanya haraka". mwendesha gari alitoa gari kwa kasi kuelekea huko ambapo raisi amepahitaji kwenda.
mara nyingi huenda kwenye nyumba hii kwa kificho kikubwa asionekane na huenda na mlinzi mmoja tu.
"Siamini anacho kisema jaji kama kinaukweri lakini nitajua tu ukweri uko wapi."alikuwa akijiwaza na kuona gari kama harikimbii sana ili wawahi kufika.
ENDELEA...................
"Jesika unajua mpaka sasa siamini kinacho endelea, yaani Raisi amekubari ombi langu hakika maajabu". Edisoni alimweleza mwanae Jesika huku akiongeza mwendo ili kuzipita gari tatu zilizo kuwa mbele yake.
"kwahiyo hajaleta hata upingamizi wowote bali amekukubaria?" Jessi aliuliza
"hapana hajaleta upingamizi wowote mimi nime mweleza kila kitu lakini baadae hajakataa ombi langu ameniambia kuwa hili atalizuia kwanza asinyongwe mtu huyu na pia lingine ameniambia kuwa inaweza kutokea waandishi wa habari wakataka kuhoji, kwanini hajanyongwa? lakini wakija kwangu basi sita hangaika bari nitakacho kifanya ni kuwaambia kwamba kuna mambo mengi ambayo yamelazimu kusitishwa kunyongwa mtu huyu." jaji alisema.
"sawa baba lakini baada ya hayo yote unataka ufanye nini kwa sababu ukizingatia kesi hii ni kubwa hawezi kuachiwa hivihivi lazima atanyongwa sasa wewe unalipi la kufanya" Jesika aliuliza.
muda kidogo ulipita jaji akijihisi furaha kubwa moyoni alicho kijibu baada ya Jessi kumuuliza ni "Jessi mimi sina utaalamu wa upelelezi nikimaanisha sikusomea upelelezi bari nilisomea sheria sasa kwangu ni ngumu sana kufuatilia na kupata ukweri wote, hii ni kwasababu tuu kuhitaji kuthibitisha kuwa walio kufa walikuwa na hatia na siyo huyu anae enda kunyongwa bali wale walio kufa," jaji alinyamanza na kuendelea
"wale watu ni waharifu sasa ili kuthibitisha ukweri wote lazima apatikane mpelelezi alie bobea ili afanye uchunguzi wa maisha waliyo kuwa wanaishi hawa watu, ukweri wote ukiwa wazi basi Esilomu hana hatia lakini bila kupata ukweri wa jambo hili basi niwazi Esilomu bado atakufa tu ila kumusaidia ni kutafta ukweri wa maisha ya hawa watu wawili yaani Ishimael Shemley na Fabiano Andrew
tukisha pata uharisia wao basi kesi imeisha lakini nibaada ya kumpata mchunguzi anae weza kubaini maisha ya hawa watu basi bado kazi ipo ila najua mungu yupo atatusimamia kama alivyo musimamia Musa kuwaongoza wana wa Isirael basi nasi atatuongoza kumpata mchunguzi.
tunahitaji mchunguzi kwa sababu hawa watu walifanya kificho kikubwa ili wasijulikane lakini naamini kwa ushirikiano tunaweza kuwa gundua." jaji alikatishwa kuongea baada ya simu yake kupigiwa
"haloo!" sauti ya upande wa pili ilisikika baada ya jaji kupokea simu.
"halooo" jaji akaitikia
"mko wapi mbona mda mrefu hamjarudi vipi kunatatizo?" Bi Heleni aliuliza
"hapana tupo njiani tunakuja usijali sawa!!"
"ok nawasubiri" Heleni alisema
na kukata simu.
"ni mama!" alimwambia Jesika
"ok sawa haina shida hii kwani situnaenda?" Jesika alisema
.
******
.*
*
*
Baada ya dakika kumi na tano Gabrieli raisi wa jamuhuri ya mungano wa tanzania akafika kwenye nyumba moja kubwa iliyo zingirwa na ukuta mrefu kwenda juu na mpana.
ni nyumba yenye hadhi kubwa hapa Dar es salaamu wengi wanadhania hakuna mtu anae ishimo.
ndani ni seheme nzuri palipo pambwa na maua ya kupendeza ambayo yalipafanya paendelee kung'a kwa uzuri wa kipeke sana.
Mwendesha gari alienda akalisimamisha sehemu maalumu ya kusimamisha magari
Raisi hakusubiri afunguliwe mulanga alijifungulia akaanza safari ya kuingia ndani ya nyumba hii ambayo kwa sasa ilikuwa kimya sana japo kuwa kunandege wadogowadogo walio kuwepo mahari hapa wakiendelea kutoa sauti zao.
alitembea kwenye velanda ndefu na kufika sebreni lakini hapakuwepo mtu yeyote mahari pale kama siyo ndege aina ya kasuku.
alienda moja kwa moja kwenye chumba kimoja kilicho kuwa kimefungiwa kwa ndani
"ali gonga gonga kwa kutumia mkono wake pale mlangoni mara tatu kisha akasema "Ni mimi fungua mlango"
"nakuja kufungua" sauti nzuri ya mwana mke ilisikika mre chumbani
mlango ukafunguliwa
"karibu sana, vipi mbona hauja nitaarifu kua unakuja" binti huyu alisema.
"samahani sana Penina" Gabriel alisema kwa kumuomba msamaha
"Usijari karibu ndani"penina alisema.
"vipi kuna mapya huko? mbona umefika gafra namna hii? Penina aliuliza.
kimya kidogo kilipita raisi akasema "Penina kwanza naomba kabla sijaongea nikuulize"
"uliza tu usijari". penina alijibu.
"Unamjua Esilomu?" Gabri
aliuliza, swari hili lilimfanya ashindwe kuongea kitu akabaki ameduwa.
"Penina nauliza tena Je,unamfahamu Esilomu?" Gabri aliuliza tena sauti hii ilionesha amedhamilia kwa kile alicho kuwa akikiongea.
"Kwahiyo umenileta tanzania kwakutaka niishi kwa huzuni? au umenileta tanzania kufanya nini maana kila kitu unacho kifanya ni kuniumiza tuu sasa ndo nauliza umeamua kuniumiza au?" penina alisema huku macho yake yakianza kutokwa na machozi.
"Penina nauliza tena kwa mara ya mwisho je,unamjua Esilomu? nijibu kama unamjua". raisi aliuliza tena
"My love naomba usikie mimi ni binti nilie ishi maisha ya shida sana miaka ishirini na nane iliyo pita nilikuwa naishi na kaka yangu ambae nilimpenda sana alikuwa anaitwa Edisoni Mwasera tuliishi sisi tu wawili baada ya wazazi wetu kufariki, hatukua na msaada ila siku moja kaka alienda kwa mku wa mkoa kuomba msaada mwisho akakubariwa na akawa amechukulliwa akaishi kwake ila mimi sikupata kokote,
sikuchache baadae alikuja mtu mmoja kutoka kule Arusha akadai kuwa anahitaji wasichana wakwenda kule mjini kufanya kazi kwenye hoteli moja kwa sababu sikuwa na kipato nikaamua niende angalau nipate chochote baada ya kwenda huko sikutegemea kumbe mtu yule alitafta wasichana wa kuuza mtu unauzwa ili yeye apate kipato yule alie kupeleka hakua mimi tu bari tulikuwa wengi wasichana tuliokuwa tunauzwa nilikuwa nauzwa ili watu watumie mwili wangu kwa starehe na ndipo ulipo nikuta najiuza kipindi kile nakumbuka na wewe ni moja wapo wa watu nilio lala nao ila baadae nilipata ujauzito nikajifungua mtoto wa kiume nikamuita jina Esilomu ila kwakuwa sikuwa na uhakika na baba yake nikaamua kumpa jina la rafiki yangu aliekuwa anaitwa Ngwale, nilifanya hivyo kwa sababu baba yake kabisa nilikuwa simujui.
mambo mengi yalifanyika nikawa nataka kujiengua na kazi ile nakutaka kujifanyia kazi nyingine lakini yaliyo nikuta ndiyo yale uliyo yaona na hata hivyo nakushukuru kwa kuniokoa mpaka sasa niko hai ndiyo maana niko tayari kwa chochote kutoka kwako.
kwahiyo hayo ndiyo yaliyo nikuta mpaka sasa sijui wapi alipo kaka yangu na wala alipo mtoto wangu hata rafikiyangu Ngwale sijui kama ni wazima au laa!!
hiyo ndiyo historia yangu kiufupi." Penina alisema huku machozi yakimtoka, Gabri alishindwa kujizuia akamkumbatia nakusema "pole sana tena sana sikujua yote hayo sasa mbona hukuniambia toka mwanzo mara tuu ulipo toka hosipitali?"
"muda wake ulikuwa bado sikutaka kukuchanganya wakati ule". penina alijibu.
"nikwambie kitu?" Gabri aliuliza
"ya! do it!!" penina alijibu
"Edisoni Mwasera bado anaishi"
"eti nini? kwani unamfahamu"penina aliuliza kwa mstuko mkubwa
"Ndiyo anaishi na habari njema ni kwamba nilipo chaguliwa kuwa raisi nilimteua kuwa jaji, nilimteua bila kujua kuwa yeye ni kaka yake na mtu nimpendae tena ninae mthamini, kwahiyo bado anaishi na nzuri zaidi mwanao Esilomu yupo hapahapa Dar na kwa kukufurahisha zaidi kesho asubuhi angalia taarifa ya habari utajua nini kinaendelea lakini wote wapo hao watu mhimu kwako". Gabri alisema huku Penina akiwa anamuangalia kwa kushangaa kinacho tokea alihisi ni ndoto anayo kuwa anaota
"hapana Gabri acha kuniweka katika wakati mgumu namna hiyo" Penina alisema
"Penina trust me!" Gabri alisema
"siwezi kuamini gabri unacho niambia"penina alisisitiza.
"leo kaka yako amekuja nyumbani kwangu na kunisimulia kila kitu kilicho wapata na kama ulikuwa hujui alie waua hawa viongozi wawili yaani makamu wangu na waziri mkuu ni mtoto wako Esilomu".
"Nini?"
"Habari ndo hiyo, kwamba alie waua hawa watu wawili ni Esilomu Ngwale na kwa sasa yupo gerezani na alie toa hukumu ni kaka yako Edisoni alitoa hukumu bila kujua kuwa ni ndugu yake ila tuu elewa bado wapo tena wapo hapa hapa Dar, mimi nataka kuondoka kunasehemu naenda ila kumbuka Gabrieli wa leo siyo wa zamani mimi nilisha badilika sasa nitamsaidia Esilomu japo kuwa simujui baba yake" Gabri alisema huku akijianda kutoka mle chumbani
alisimama na kuanza kutembea kuuelekea karibu na mlango
"Gabri rudi kidogo.." Penina alisema.
alirudi na kusikiliza mambo ambayo anataka kuambiwa na penina.
"Gabri kama yupo Esilomu tafadhari nakuomba umpimishe vina saba vya damu yawezekana ni mtoto wako" Penina alisema
"unasemaje Penina?" Gabri aliuliza
"Ndiyo nimesema kwa kumaanisha.
pindi nilipo pata ujauzito hata wewe tulilala wote kwahiyo inawezekana Esilomu akawa mtoto wako"
Gabri hakuamini kabisa kusikia hivyo alimwambia penina
"penina nakupenda sana nakuthamini natena kama unavyo jua kuwa sina mtoto, siwezi kuamini nikija kujua kamba Esilomu ni mwanangu hakika siwezi amini haya yote lakini ngoja nikuache niende kushughulikia suara hili kwanza la Esilomu.
naenda ila pia nitapita kwa Edisoni ila sitamwambia chochote maana muda bado haujafika wa kuambiwa". Gabri alisema huku anainuka na kutaka kuondoka
aliinama na kumnong'oneza
"kama Esilomu ni mwanangu nakuahidi kufanya jambo laajabu ambalo watanzania watashangaa".
alimaliza na kuondoka
"haiwezekani eti Esilomu yupo? Edisoni yupo? Wako hapahapa dar es salaam? nitawapataje? ila ngoja nitaona kama ni kweri kuhusiana na swara hili."Penina alijiwaza huku akishika shavu lake la kuume kwa kutumia mkono wake wa kuume.
"Mungu wangu wewe mwenyewe unanijua Gabriel wa sasa si yule wa zamani mimi nilisha badilika sana ila kama huyu ni mwanangu nifunilie ili nijue hee kama ni yeye nitafanya sherehe kubwa sana sito amini kitakacho kuwa kimetokea ni ndoto nadhani hii ninayo iwazia haiwezekani Esilomu awe mwanangu nilitembea nae Penina siku moja haiwezekani mimi nikawa ndiye nilie mpa mimba lakini yote kwayote lazima nihakikishe kwanza kwa kupima vina saba vya damu ndipo nitajiamini ila kwa muda huu nielekee kwanza kwa jaji ili kumtaarifu kwamba sasa naelekea kutuma barua ya kutaka isitishwe zoezi la kumnyonga Esilomu mpaka pale ukweri utakapo patikana.
Gabrieli alikuwa akijiwaza huku gari linaelekea kwa jaji.
baada ya dakika chache alifika kwa jaji Edisoni
gari liliingia getini na jaji akashangaa kumuona raisi amekuja kwake haikuwa rahisi raisi kufika kwa mtu kama huyu na huku hana walinzi wake kama ilivyo zoeleka.
"aa karibu sana mkuu"jaji alisema akiwa anamkaribisha ndani
"asante sana" Gabri aliitikia akaingia ndani
"karibu sana"mke wake Edisoni Bi heleni alimkaribisha
"asante sana shemeji" Gabri alisema.
"unatumia nini? soda au?" Jesika aliuliza
"hapana wewe usilete chochote"
kabla hajamalizia mlinzi wa jaji Edisoni akaingia na kutoa taarifa kwamba
"mkuu kuna mgeni amekuja anahitaji kukuona vipi nimuruhusu aingie?" mlinzi aliuliza.
"ninani?" jaji aliuliza.
"amejitambulisha kuwa ni Dakitari Vijey Shaluma" jaji alistuka sana yeye na mke wake wakaangaliana ,
"umesema Daktari Vijey Shaluma?" jaji aliuliza.
"ndiyo" mlinzi alijibu.
"mwambie asubiri nakuja" jaji akasema huku moyo ukimuenda mbio kwa kitu alicho ambiwa.
alimwangalia mkewe kisha akaangalia chini akasema kimoyomoyo "haiwezekani dakitari Vijey Shaluma amekuja huku tanzania? kwa nini? Vijey siwezi kukubari utoboe siri niliyo itunza sikunyungi zilizo pita haiwezekani" jaji alihisi maji mwilini baada ya kijasho chembamba kumtoka.
ITAENDELEA......
FUATILIA KISA HIKI CHA KUSISIMUA
LIKE AU SHARE AU COMMENT ILI TUWE WOTE PAMOJA.
HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 6
HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 6
HUKUMU YA HAKI
SEHEMU YA..6
Mtunzi Ayubu Henry
ILIPOISHIA....
Jesika alimuangalia babayake alie kuwa ameshika usukani vyema.. binti huyu aligundua kuwa hakika baba yake alikuwa akimaanisha kile alicho kuwa akikiongea.
"Nilazima Esilomu nimsaidie kwa tatizo hili aliro naro, kwanza ni ndugu yangu ni mtoto wa dada yangu ila harafu niwajibu wangu kusimamia sheria lazima haki itendeke siwezi kumuacha kabisa afe nikiwa naona ni mtu wa muhimu kwangu, nadhani nikifanya mchakato kesho asihamishwe na kesho kutwa asinyongwe basi nitakuwa nimefanya vizuri itanibidi nifanye uchunguzi kuhusu maisha ya hawa watu wawili ndipo nitakapo kuwa nimempa uhuru Esilomu kinyume na hapo atanyongwa tuu, siwezi kuruhusu hili dada yangu alikwenda ila mwanae hawezi kwenda kingali nipo hai..". jaji alikuwa akijiwaza huku akiwa anaendesha gari kwasi kuelekea ikuru kwa raisi wa jamhuri ya muuangano wa tanzania.
ENDELEA.......
Munamo saa sita na dakika ishirini na mbili Jaji Edisoni alifika ikuru kwa mheshimiwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania mheshimiwa Gabrieli Musa.
walipokelewa na walinzi pale inje ya geti kubwa walinzi wale waliwasongeza mpaka geti la pili katika geti hili walipokelewa na vijibaba ambavyo kwa kawaida ungesema ni wapambanaji wa ulingoni au ungesema ni wakaza misuri.
"Samahani walinzi vipi kweri nimemkuta mheshimiwa?" jaji aliuliza kwakuwa alikuwa anaheshimika alijibiwa tofauti na watu wanao kuja nakuuliza kisha wasijibiwe.
"ndiyo yupo" ilikuwa sauti nzito kutoka kwa mrinzi mmoja wa mheshimiwa raisi.
"vipi yumo ndani au kule nje sehemu ya kupumuzikia" jaji aliuliza kutaka kupata ufafanuzi wa kina kuhusu alipo kuwa raisi.
"yupo kule bustani kwahiyo ukimtaka nenda kulekule" mlinzi yule alijibu.
"sawa nashukuru, Jesika Twende".
waliongozana mpaka wakafika bustanini
"karibu.. .....karibu sana, jaji vipi bwana za nyumbani huko?" Mheshimiwa Gabrieli aliwakaribisha
"asante sana na nimesha karibia , huyu unae muona hapa ni mwanetu yule mdogomdogo wa siku zile sasa amekua siyo mdogo tena" jaji alisema.
"anaitwa nani nani.....nani Jesika?" raisi alihoji.
"ndiyo kabisa" kabla jaji hajamaliza Jesika akamuamkia raisi "shikamo mzee?" jesika aliamkia
"marahaba!!!! haujambo mama?" raisi aliuliza
"mimzima kabisa mungu anasaidia, maana ni wengi walio tamani kufika siku ya leo lakini hawaja weza ila mimi bado nipo shukulani kwake alie juu" Jesika alisema.
muda mchache ulipita baada ya jaji kufika ikuru, alionekana ana kitu cha kuongea lakini alisitasita kusema.
Raisi akaanza "Ndiyo jaji majukumu ya kifamilia yakoje na vipi nasikia unashikilia vyema sheria, ila nikupongeze kwa juhudi zako za kusaidia tanzania maana bila mahakama hakuna sehemu nyingine penye mamulaka ya kuhukumu ni mahakama tuu, hakika nyie ni wa mhimu katika kusimamia sheria, tunahitaji watu kama nyie" Gabrieli hakumalizia akaambiwa na mmoja wa walinzi wake kuwa simu yake kunamtu amepiga aliomba musamaha kwa jaji na kutaka kuzungumza na mtu simuni, ali toka pale walipo kuwa wame kaa na kuzungumuza na mtu yule aliekuwa amempigia.
"sasa Jesika nakuomba unisubilie hapo nje kuna mambo ya muhimu tunayo taka kuongea mimi na raisi hasa kuhusuEsilomu kwahiyo naomba unisubiri hapo nje, muda si mrefuvnitakuja sawa?" Eddi alimwambia Jesika na baada ya muda wa dakika nne raisi alirudi
"Eddi samahani kwa kuningojea alie kuwa amepiga ni mtu wa mhimu sana hivyo nakuomba ladhi kwa kujari simu na kukuacha hapa!" raisi alisema.
"hakuna tatizo mkuu wala usinihofie kabisa mkuu,"Edisoni alisema
"sawa, ehe vipi lakini unatumia kinywajigani?" mheshimiwa raisi aliuliza.
"aaaa hapana mkuu sijisiki kupata kinywaji". jaji alijibu.
"aaaaaaaaa wewewewe, hapa ni nyumbani Eddi jisikie upo kwako kabisa tena jisikie uko nyumbani kijana wangu!!!" Raisi aliongezea.
"Nashukuru sana mkuu".Eddi alisema..
"kwani vipi ndugu kuna tatizo mpaka hata kinywaji usitake??" Raisi aliuliza.
"Ndiyo lipo" eddi alijibu
"lipi tena".
"nikubwa kiasi, lakini nimekosa sehemu ya kwenda nikaamua nije kwako angalau kutafta msaada na nadhani hapa ni sehemu sahihi". Eddi alisita kido harafu akaendelea.
"mkuu kwakweri sina mtu alieko juu mwenye kunisaidia kwa hili."
"sawa wewe sema hapa ni nyumbani na kama nilivyo tangulia kusema ni kwamba jisikie uko nyumbani, kuwa huru kabisa kijana wangu,
wewe ni moja kati ya vijana wanao tegemewa katika ujenzi wa taifa." Raisi alisema huku Jaji Eddi akijianda kusema lililo mleta pale japo kuwa bado alikuwa na kigugumizi kikubwa kwa kuhofia kuwa Raisi asinge kubari ombi lake kwa sababu upana wa kesi ya Esilomu ni mkubwa mpaka ilimtia shaka kubwa sana alipo kuwa anakumbuka kwamba alie kufa ni waziri mkuu wa mambo ya ndani na makamu wa raisi, tena makamu wake huyuhuyu raisi alieko madarakani.
alijikaza mwisho akasema.
"mheshimiwa sikupenda kukupotezea muda, lakini nitatizo lenye upana mkubwa sana ila ninakuomba unisikilize kisha uangalie wapi pa kunisaidia."
alinyamanza kidogo kisha akaendelea.
"mimi naitwa Edisoni Mwasera nililelewa na mtu ambae si baba yangu, baba yangu na mama yangu walifariki takiribani miaka 28 iliyo pita, niliishi na dada yangu yaani anae nifata kuzaliwa, familia ya mzee Mwasera ilibahatika kupata watoto wawili tu yaani mimi na dada yangu.
maisha yalitubana sana mimi na dada yangu baada ya baba na mama kufariki tukaamua kusambaa kwenda kutafta musaada sehemu nyingine, mimi nilibahatika kupata nafasi ya kuishi na mkuu wa mkoa wa kipindi kile
lakini mdogo wangu yaani huyo binti siku moja alinitumia ujumbe yaani barua fupi ikisema yeye alipata kazi ya kuweza kumdu maisha aliyo kuwa anaishi, alicho kidai ni kwamba alipata mtu wa kumuajiri kwenye hoteli moja kule Arusha, alipelekwa na yule mtu kumbe masikini yule mtu hakuwa na roho nzuri
alimpeleka na kuanza kumuuza dada yangu akawa anatumikishwa kama mnyama,
alikuwa anauzwa kwa wanaume watumie mwili wake na mtu alie kuwa akimwajiri alihakikisha kwamba anajipatia masirahi kupitia mwili wa dada yangu.
mwisho wa siku alibahatika kupata mtoto ila baada ya kupata mtoto dada yangu hakumjua baba yake yule mtoto kwa sababu alikuwa ametembea na watu wengi kwahiyo ilikuwa ngumu kumjua baba harisi wa mtoto yule ni nani.
Baada ya siku chache dada yangu ikasadikika kafa na mtoto yule akakosa msaada japo kuwa alilelewa na mzee mmoja ila hakumkidi mahitaji yake ya msingi kama vile kumsomesha ne mengine mengi mwisho wa siku akajiingiza katika vikundi vinavyo sambaza bangi na aina nyingine ya madawa ya kulevya, kazi hii ameifanya chini ya mtu mmoja ambae mwisho alimuzurumu lakini kijana huyu baada ya yote hayo aliamua kulipiza, moja alianzia na alie muua mama yake yaani dada yangu na mwisho akamuua mtu alie mzurumu pesa baada ya kufatilia malipo na kukosa." jaji alionekana amemaliza ila chozi lilimtoka alipo kuwa akiwaza mateso ambayo dada yake aliyapata kama kila siku lazima atumiwe na wanaume watano au mpaka saba tena kikatili kwa kulazimishwa na pia kila siku ilimbidi afanye kazi hiyo ambayo alikuwa analipwa kidogo sana au asilipwe kabisa hakika alitoa chozi.
"pole sana Eddi kwa matatizo yaliyo kukumba na kukufanya uumie tena uteseke, eddi hii nilazima binadamu apitie kwenye maisha yake unaweza kudhani uko peke yako pindi unapo patwa na tatizo unadhani dunia yote umeumbiwa wewe tuu lakini hata mafundisho ya biblia inafundisha tuwe na uvumilivu, kwa hiyo usijari sana, mimi mpaka nafika hapa nimepitia mengi mno tena mengi sana ambayo leo hii nikikwambia huwezi kuamini ndiyo maana leo mimi watu wenye matatizo nawasaidia ni kwa sababu najua niliko toka na laiti viongozi watakao fata na waliomo madarakani wangeliona hili wakaamua kutumia pesa zao kwa ajiri ya kusaidia na siyo kwa ajiri ya siasa hakika tunge endelea. Lakini kama raisi wa nchi hawaniungi mkono napojaribu kutafta msaada wa watu ambao hawajiwezi hakika hatuwezi kufika". Gabrieli raisi mwenye busara alimweleza Edisoni.
dakika chache kupita Raisi akauliza "sasa Edisoni nikusaidie wapi, kweri umesema tatizo lakini je unataka msaada gani kutoka kwangu.?"
Edisoni akaangalia chini nakusema "mkuu huyu kijana ninae mzungumzia kwa sasa yupo jera amesubiri kunyongwa, alie toa hukumu ni mimi mwenyewe lakini kwa shinikizo la viongozi wa juu ndo maana nikatoa hukumu ile".
"jina lake nani?" Raisi aliuliza kutaka kumjua.
"ni huyu Esilomu Ngware"
"huyu alie muua makamu wangu au?" raisi aliuliza
"ndiyo na mama yake ni binti mmoja alie kuwa dada yangu nae anaitwa Penina Mwasera" jaji alisema.
"weee Penina Mwasera?" raisi akauliza
"ndiyo Penina Mwasera ni dada yangu" jaji alijibu.
"etii Penina Mwasera?? Penina huyuhuyu ninae mjua au? ha!
haiwezekani kabisa Penina Mwasera eti ni dada yake na Edisoni?" Raisi aliwaza huku moyo ukimuenda mbio.
"kwani unamfahamu Penina Mwasera?? binti huyu alisha kufa siku nyingi zilizo pita". jaji aliuliza na kumueleza Raisi.
"aa!a! poleni sana na pole sana kwani unataka nifanyeje ili kukusaidia?" raisi aliuliza.
"ninacho taka nikwamba Esilomu asinyongwe bali kesi isubiri ukweri na mwisho uandaliwe huo ukweri ufikishwe mahakamani ili ionekane haki iko wapi je anyongwe Esilomu au aachiwe!!."
"Edisoni nimekuelewa najua cha kufanya wewe nenda nyumbani nitazuia asinyongwe na baada ya kuzuia asinyongwe tutaangalia jinsi nyingine ya kufanya".
"siamini kabisa" jaji alisema.
" wewe amini sawa jaji?" Raisi alisema japo kuwa Jina la Penina liliendelea kumfanya ashindwe na mazungumzo akawa anaongea kwa kukata kata maneno.
"sina shukurani ya kukupa mheshimiwa ila mungu atakurudishia ni yeye ampae yeyote kitu chochote tumuombacho" jaji alishukuru hakuamini kabisa alihisi ni ndoto aliyo kuwa anaota wakati ule
"wewe nenda nyumbani nadhani kesho asubuhi utasikia taarifa kwenye redio hii ya tanzania au tbc1 na vyombo vingine kwenye yaliyo jili na nadhani wandishi wa habari watakuja kwako kupata mawili matatu kutoka kwako". raisi alisema.
jaji alishukuru nakuagana na mheshimiwa raisi tayari kuanza safari kurudi nyumbani.
"Haiwezekani eti Penina Mwasera ana mtoto tena ni mtu alie saidia kuiokoa tanzania he! mbona sikulijua hili mapema ngoja nifatilie kwanza sababu haiwezekani". raisi alikuwa anajiwaza huku akieleka sehemu ambapo magari yana pakiwa na kufunguliwa mlango akamwambia mwendesha gari
"naomba twende Nyumba namba H2029 balabala namba 32 fanya haraka". mwendesha gari alitoa gari kwa kasi kuelekea huko ambapo raisi amepahitaji kwenda.
mara nyingi huenda kwenye nyumba hii kwa kificho kikubwa asionekane na huenda na mlinzi mmoja tu.
"Siamini anacho kisema jaji kama kinaukweri lakini nitajua tu ukweri uko wapi."alikuwa akijiwaza na kuona gari kama harikimbii sana ili wawahi kufika.
ITAENDELEA....
TUKUTANE SEHEMU IJAYO
LIKE NA COMMENT ILI TUWE WOTE.
HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 5
HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 5
HUKUMU YA HAKI
SEHEMU YA..5
Mtunzi Ayubu Henry
ILIPOISHIA....
umesema kuwa ni Penina Mwasera?". jaji aliuliza.
"ndiyo, kwani unamfahamu?"
eddi aliuliza.
"Ndiyo namjua tena namjua".
Edisoni alisema akiwa anatetemeka na machozi yakimtoka.
"namjua....namjua.... namjua
Penina Mwasera namjua kabisa namjua kabisa namjua"
jaji aliendelea kusema kwa pupa huku machozi yakichuruzika na akiwa anaria
kitendo ambacho kilimusisimua kila mmoja pale nakushangaa na kupata shauku la kujua nini kinaendelea na kumjua huyo Penina Mwasera
ENDELEA......
"baba kwani huyo penina ni nani" jesika aliuliza.
"mwanangu unataka kumfahamu huyu Penina" Eddi aliuliza.
"Hapo nyuma kidogo kama miaka 28 iliyo pita kuna mambo mengi yaliyo tokea kijijini kwetu wasichana baada ya kukosa shule wengine walianza kwenda kigoma mjini na wengine mikoa mingine kwenda kutafta pesa za kuwa tunza, wakati huo walitoka wasichana wengi sana,
siku moja nikiwa na dada yangu tulikuwa tumekaa sehemu tunajaribu kupangilia tufanyeje kwa sababu wakati huo tulikuwa hatuna wazazi tulikuwa yatima,
wazazi wetu walifariki mwaka mmoja ulio kuwa umepita kwa wakati ule.
Mama yetu aliitwa Jesika Andrew na baba yetu aliitwa Mwasera,
jina mwasera lilitokana na wazazi wake walio muza yaani babu na bibi zetu
babu aliitwa Mwamuzi Isaya na bibi aliitwa Selina Rashidi
walichukua majina yao la baba na la mama wakajumlisha vyanzo vya majina yao baba walichukua Mwa na mama wakachukua Se na mwisho wakaongeza Ra wakapata Mwasera.
ila nasikitika kuwa nasikia habari zao wala sikuwahi kuwaona nao nasikia walisha kufa.
siku hiyo tulivu tulikuwa tunajaribu kufikiria tufanye nini tukashauriana kuwa tusambae mimi niende kwa mkuu wa mkoa kuomba musaada kweri mimi nilienda kuomba musaada kwakuwa mkuu yule bwana Aridi Yusufu mkuu wa mkoa miaka ile
hakubahatika kuzaa alinichulia kama mtoto akaamua kunisomesha.
muda mchache ulipita dada yangu alinitumia barua nayo hii hapa huwa kila napoenda naendanayo barua hii imeandikwa.
Kwako kaka mpendwa Edisoni, najua kuwa hautapenda kukaa mbari na mimi lakini itakulazimu ukae mbari nami,
mimi nimekaa nakuwaza nimeamua kwenda mjini kutafta maisha na kuna mtu kaja kunichukua anasema ananipeleka kufanya kazi hotelini, nafikiri nikienda kule naweza kupata pesa na baadae nikaendelea kiuchumi.
naenda Arusha japo kuwa bosi simujui ila naenda kule kwa kupelekwa na mtu kutoka hukohuko Arusha nadhani ni mtu alie tumwa kuja kutafta watu wakuweza kuwasaidia.
namaliza kwa kusema nakupenda sana.
wako mpendwa Penina Mwasera."
jaji aliwasomea huku akihisi kupasuka kwa sababu ya musongo wa mawazo na kutetemeka.
baada ya kuwasomea akaendelea
"baada ya mda mwingi kupita niliona vema kuweza kwenda Arusha kumtafta dada yangu rakini sikumpata nilijitahidi kutafta kila hoteli lakini sikumpata.
Baada ya muda tulihamia Dar tukaishi huku nikaamini kuwa dada alisha kufa na itakuwa ngumu hata wa kujua alifia wapi.
miaka mingi imepita kumbe wewe ni mpwa wangu??
mtoto wa dada yangu??
Essi njo mwanangu unikumbatie mimi na wewe ni familia moja wewe ni familia yangu".
walikumbatiana wote wakiwa wanalia
kila mmoja hakuamini kumbe Esilomu ni mtoto wa Penina dada yake Edisoni hakuna alie kuwa analijua hilo,
walikumbatiana wote wawili yaani Esilomu na Edisoni kila mumoja analia akisema "siamini ....siamini."
Dakika tano zilikatika wakati wakiwa wote wanakumbatiana kumbaiana kwa uvhungu.
jaji alisema
"Essi usijali wewe ni familia yangu siwezi kukuacha upotee kama alivyo potea mdogo wangu Penina nikiwa naona, niko tayari kukusaidia usijari mwanangu, wewe ni sawa na mwanangu" jaji alisema huku machozi yakimutoka.
baada ya kusema yote hayo akasema "Essi bado siku mbili ili wewe unyongwe lakini niko tayari kukusaidia na tena niko tayari kukupeleka sehemu yeyote ili uwe huru.
ila nakuomba uniache nikajaribu kutafta mbinu ya kukusaidia, sababu ukweri nimesha upata wewe usijari,
kesho utatoka humu jera by any means".
alimaliza akiwa anaamka na kuanza kutembea huku nyuma akimfata Jesika, mda wa dakika mbili na sekonde kadha walifika kwa bwana jera.
"ndugu yangu ninajambo la kuongea ila ni kwaajiri yangu tuu na wewe, je tunaweza kutoka kidogo?" Jaji aliuliza
"ndiyo usijari wewe ni kama ndugu nikikumbuka ulivyo nisaidia mambo mengi kwa nini nisikusilikilize?" bwana jera alisema.
"jesika naomba ubaki hapa tunakuja dakika sii nyingi sawa baby?" baba alisema.
"ok dady" Jesika alisema huku Edisoni na bwana Jera wakielekea nje kwa mazungumzo.
Wote walikuwa kimya kama dakika mbili ndipo bwana jera akauliza "Ndiyo" aliashilia kutaka kujua zaidi kinacho msibu Edisoni.
nae eddi hakusita akasema "ndugu yangu kuna jambo ambalo naweza kusema ni kubwa kuzidi mamlaka yangu na pia kuzidi kabisa ufikiliaji wangu" Eddi alinyamanza na kuendelea
"nakosa hata nianzie wapi ndugu yangu kukuelezea, sababu ni jambo zito sana".
bwana jera akasema baada ya edisoni kuwa na kigugumizi kikubwa kulingana na tatizo lake."jaji wewe nikama ndugu yangu tumesaidizana mengi maishani sidhani kama matatizo yako kuwa hayani husu, yananihusu kabisa wewe niambie....." hakumalizia Edisoni akadakia nakusema.
"ndugu yangu kama unavyo jua sina baba wala mama ninaishi hivihivi nilivyo,
miaka takilibani ishirini na nane nilikuwa naishi na dada yangu, aliitwa penina nilimpenda sana!! sikupenda akae mbali nami, najua lilikua jukumu langu la kumulinda dada yangu ila sikufanikiwa mara tu baada ya kuchukuliwa na mtu wa kunilea na kutaka kunisomesha dada yangu alinitumia barua, najua barua ile hakuandika yeye aliandikiwa kilicho nifanya niumie zaidi ni pale milipo kumbuka dada yangu hajui kusoma lakini kanitumia barua, siwezi nikaitupa nitatembea nayo mpaka kifo changu" jaji alinyamanza kidogo huku akijifuta machozi ambayo yalikuwa yameanza kuchirizika akaendelea na simulizi ambayo imeanza kumuingia bwana jera.
"barua hiyo ilinijulisha kwamba yeye dada yangu amepata mtu wa kumpeleka Arusha kwa shughuri moja ya Hotelini, yaani kama kufagia na mambo madogo madogo yaani zile kazi ambazo mtu ambae haja soma anaweza kufanya. sikuweza kumzuia kwa sababu sikumuona hiyo ilikuwa mara yangu ya mwisho kumusikia tena wala kumuona.
miaka kadha nilienda Arusha wakati hatujahamia huku dar es salaamu. Nilifika kule Arusha kumtafta dada yangu lakini sikumpata takilibani kila Hoteli kubwa niliingia lakini sikumpata, hivyo nilikaa nikiwa najua kuwa dada yangu sito muona tena, ila reo sijui kwa nini hili limetokea mtu alie shikiliwa na polisi kwa mauaji na mwisho akakosa hata ndugu wa kumsimamia katika kesi yake kumbe ni mtoto wa dada yangu.
dada yangu kabisa ndiye mama yake Esilomu Ngware mtuhumiwa kwa makosa ya uuaji wa watu wawili vigogo." jaji alisema huku akiashiria kuna mengi yanamuhusu Esilomu.
bwana jera hakuamini alihisi anaota kwa yale aliyo ambiwa "kumbe Esilomu ni ndugu yake Edisoni? hii ni ajabu sana, kwakweri mungu ni waajabu sana yaani watu walio poteana wanakuja kujuana kwenye shida mungu wewe ni waajabu"bwana jera alijiwaza huku akimuangalia jaji aliekuwa anajifuta machozi ya furaha na maswari mengi.
mda mchache kupita bwana jera akauliza "sasa ndugu yangu kwanza pole na matatizo yaliyo kusibu ila napenda kukupa pole ila pia asante kubwa ni kwa Mungu alie juu maana yeye ndiye alie panga hili litokee na kama alivyo panga basi ni suara la kujua pia atamaliza yeye mwenye mungu.
ila pia nasikitika kukwambia kwamba kesho Esilomu Ngware atahamishwa kupelekwa jera nyingine ambapo hupelekwa watu maarumu kama wanao nyongwa au wenye kifungo chamaisha." Jaji alistuka sana baada ya kuambiwa kesho inatakiwa ahamishwe Esilomu kupelekwa sehemu nyingine.
"kwani atapelekwa wapi?" eddi aliuliza
"huturusiwi kupasema wala kusema siri hii ila ninaweza kukuambia usijari ila kwa maelewano kwamba hutasema." bwana jera alisema baada ya kusema jaji akadakia "najua lazima mfanye siri lakini naomba nikuulize kitu kimoja inamaana huko atapelekwa saa ngapi?"
"hawana muda maalumu ila mala chache huwa wanawapeleka saa nne za asubuhi ila mala nyingi huwapeleka saa kumi na mbili arufajili , kwa hiyo siwezi kujua moja kwa moja atapelekwa saa ngapi.
lakini Eddi naomba niurize"
"uliza tuu" jaji alijibu.
"kwa maelezo yake nikweri kwamba aliua?" bwana jera aliuliza.
"ndiyo aliua , hakika yeye ni muuaji ila ana sababu!!!" jaji alijibu.
"zipi hizo sababu?" bwana jera aliuliza
"ndugu yangu natamani kukuambia lakini nihistoria ndefu huu siyo muda wake nitakuambia ngoja nifanye kwanza mchakato wa kumsaidia kwanza kijana huyu". alisema huku wakiwa wanarundi ndani ambapo walimuacha Jesika,
walikuta jesika anabadilishana mawili matatu na walinzi walio kuwepo pale.
"sasa unaenda wapi kwa sasa?" bwana jera aliuliza.
"naenda kwa majaji wenzangu kuwaeleza habari hizi kwa sababu mimi nahitaji kunyongwa kwake kusitishwe harafu nitatafta namna ya kufanya upelelezi kisha niuweke wazi ushenzi na uchafu ulio kuwa unafanywa na hawa vigogo wawili ambao walionekana watu muhimu kumbe ni simba mwenye ngozi ya kondoo."
maneno yale yalimfanya bwana jera aamini kitu moyoni mwake kwamba yawezekana kunasababu ya yeye kufahu na kuwajua kiundani hawa vigogo wawili walio kufa.
Baada ya mazungumuzo machache baina ya jaji na bwana jera waliagana na jaji kutaka kuondoka bwana jera akasema " nakutakia majukumu mema yenye mafanikio"
"nashukuru ndugu yangu nadhani tutaonana wakati mwingine" jaji alisema wakaanza safari.
wakiwa safarini Edisoni hakuongea kitu ila baada ya dakika chache Jesika binti mwenye uzuri wa kipekee, binti mwenye shingo la twiga sauti nyororo akasema "baba kwani tunaelekea wapi kwa sasa?"
"mwanangu tunaelekea ikuru kwa raisi" jaji alibu
"ikuru baba?"
"ndiyo tunaenda ikuru" Eddi ali sisitiza swala hili
Jesika alimuangalia babayake alie kuwa ameshika usukani vyema.. binti huyu aligundua kuwa hakika baba yake alikuwa akimaanisha kile alicho kuwa akikiongea.
"Nilazima Esilomu nimsaidie kwa tatizo hili aliro naro, kwanza ni ndugu yangu ni mtoto wa dada yangu ila harafu niwajibu wangu kusimamia sheria lazima haki itendeke siwezi kumuacha kabisa afe nikiwa naona ni mtu wa muhimu kwangu, nadhani nikifanya mchakato kesho asihamishwe na kesho kutwa asinyongwe basi nitakuwa nimefanya vizuri itanibidi nifanye uchunguzi kuhusu maisha ya hawa watu wawili ndipo nitakapo kuwa nimempa uhuru Esilomu kinyume na hapo atanyongwa tuu, siwezi kuruhusu hili dada yangu alikwenda ila mwanae hawezi kwenda kingali nipo hai..". jaji alikuwa akijiwaza huku akiwa anaendesha gari kwasi kuelekea ikuru kwa raisi wa jamhuri ya muuangano wa tanzania.
ITAENDELEA........
MPENZI MUSOMAJI ENDELEA KUFUATILIA KISA HIKI CHA KUSISIMUA.
LIKE NA COMMENT.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO SWARI JE EDISON ATAWEZA KUMSAIDIA ESILOMU
HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 4
HUKUMU YA HAKI SEHEMU YA 4
HUKUMU YA HAKI
SEHEMU YA..4
Mtunzi Ayubu Henry
ilipo ishia .
. mimi nilimuuliza maisha yake yako nilidhani nimafupi kumbe marefu sana na pale alipo hana wazazi na hamjui baba yake nawala hata mama yake mwenyewe hakuwahi kumwambia mwanae kuwa baba yake ninani maana alikufa kingali Essi ana umri wa mwaka mmoja ilikuwa mwaka 1989 ndipo mama yake alipo faliki kuhusu jina la mama yake hajaniambia lakini alisematena kwamba mama yake alikuwa ni kahaba alipo kufa alichukuliwa na mzee mmoja anajulikana kwa jina la Ngwale alimulea ila pia yule mzee alikufa kwa mazingira ya kutatanisha na historia yake huyo mzee nikwamba alikuwa ni shoga" Heleni na Jesika walishituka sana washawishika kumjua zaidi huyo Esilomu
aliwaeleza yote na ahadi ya yeye kukutana tena kesho aendelee kusimulia historia yake na kwa nini aliua, Jesika akasema "baba naomba na mimi kesho twende wote nikamuone je ukotayari"
mzee akafikiri kisha akatoa jibu kuwa kesho wataenda wote wawili.
ENDELEA...
Siku ya tatu toka hukumu itolewe yaani tarehe 23 mwezi wa aprili asubuhi siku hii palikuwa pametulia kabisa wana dar wakiwa katika mahangaiko yao wakijitaftia riziki, kila mmoja alionekana mtu mwenye matarajio ya kwenda mahari na kufanya kazi,
asubuhi hii nimoja kati ya asubuhi zinazo muogopesha sana Esilomu Ngwale ambae kulingana na hukumu inasema tarehe 25 mwezi aprili mwaka 2014 atanyongwa kwa kosa la kumuua makamu wa raisi na kumuua waziri wa mambo ya ndani alijiuliza sana akiwaza kulingana na habari kutoka kwa jaji Edisoni kuwa yuko tayari kumusaidia.
asubuhi ya saa mbili na nusu kutokana na saa iliyoko ukutani pale nyumbani kwa jaji
wakati huu jaji alikwisha jiandaa ili aweze kuelekea moja kwa moja huko jera kwenda kumalizia historia ya Esilomu
jaji akauliza " Jesika...? Jessi mama!!!"
"bee baba!!".
"ulisha maliza kujianda". baba aliuliza.
"ndiyo nilishamaliza" Jesika alijibu huku akiwa anafungua mlango wa chumba chake..
leo binti huyu alivalia mavazi mazuri ya hadhi ya juu sana nibinti mwenye mvuto wa hari ya juu kabisa kiasi kwamba ukimuona utadhani ni moja kati ya mis tanzania.
walimuaga mama yaani bi Heleni nakuondoka wakiwa njiani walianza kubadilishana mawazo " sasa baba kunakitu nilijiuliza jana usiku" jessi alisema.
"kuhusu nini? kuhusu hii kesi au nini?!" baba aliuliza
"ndiyo kuhusu hii kesi" jesika alikubari
"ulijiuliza nini?". baba aliuliza
"nilijiuliza kwamba hapa wanao jua ukweri wa mambo kumuhusu Essi ni sisi tuu na siku zinaisha reo tarehe 23 kesho 24 kesho kutwa 25 na hii tarehe 25 atanyongwa saa sita mchana baba wewe utafanya nini kumsaidia?" jesika aliuliza swari ambalo likawa gumu kwa jaji Eddi alinyamanza kidogo nakusema "mwanangu sijui nitafanya nini lakini najua lazima nitumie kila mbinu ili niweke mambo sawa, hukumu anatoa mimi ilapia ninamamulaka japo siyo ya kufuta kesi ila ninamamulaka nitayatumia halafu nione nikishindwa kunanjia moja tuu nitakayo fanya". Eddi alisema
Jessi pia akasema "aya baba mimi sina neno la kuongea zaidi"
waliendelea na safari huku wakiwa wanabadilishana mawazo.
Ni saa nne na dakika kumi na mbili kwa mjibu wa saa iliyo ndani ya gari yao saa hii walifika magareza,
moja kwa moja wakaenda kuonana na bwana jera
ndugu Shabani Rashid.
"karibu sana jaji" bwana jera alisema
"asante sana ndugu yangu" Eddi alisema
"vipi na huyu nani?" Shabani aluuliza akimunyoshea kidore Jesika
"Anaitwa jesika ni mwanangu alikuwa urusi kimasomo sasa karudi jana, Jesika huyu ni bwana jera wa hapa".
"nafurahi kumjua shikamo mzee?" jesika alisema.
"marahaba mwanangu tupo sana tupo mpaka nyumbani kwangu!!"bwana jera alisema huku akimuangalia Edisoni.
"Tutafika usijari kwa hata kule kwako ni nyumbani kwetu" jaji alisema .
muda kidogo kupita jaji akaongezea " vipi yule kijana naweza kumpata"
"yaa yupo mnaweza kwenda kumuona yuko kule kule ulipo muona jana!" bwana jera aliwaambia.
"tunashukuru sisi ngoja tufikepo". eddi alisema.
Baada ya dakika chache walifika alipo kuwa Esilomu Ngwale, muda huu alikuwa amejilaza mara akasikia sauti ya mulinzi akiwafungulia mlango Eddi na mwanae Jessi
Edison alishangaa sana kuona uzuri wa Jesika alio kuwa nao alishindwa kujizuia alianza kuuliza " huyu na..." hakumaliza jaji akasema ni mwanangu alikuwa huko urusi kimasomo kaja jana".
"ahaaaa sawa vizuri sana, binti habari?" Eddi alisema
"poa, pole na matatizo yaliyo kukuta mpaka uko hapa, jana baba aliniambia yote yaliyo kusibu nikashawishika nifike ili nami kwa kushirikiana na mzee tuone jinsi gani ya kukusaidia". Jesika alisema kwa kumkatisha mengi ambayo Eddi alitaka kuongea na kwa sababu ya jinsi alivyo kuwa akimuangalia.
"tusipoteze muda naomba basi utuelezee je, huyu jama kwa jina la Ishimael Shemley ambae alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani,
naomba uniambie kwa nini nae ulimuua tafadhari endelea kusimulia".
"jaji nakuomba hata nikinyongwa hizi zote siri uziseme kwamba kwa nini niliua tafadhari nakuomba useme najua kuna uwezekano wa mimi kufa hata nikifa basi usisite kusema ukweri, ila usije ukasema kuwa sijaua wewe sema ila tuu nakuomba sema na sababu zilizo sababisha mimi kuua". eddi alisema huku macho yakianza kutokwa na machozi.
"usijari nitakusaidia eddi sawa?" jaji alisema.
huku akiwa analia eddi akaendelea na historia.
" Ishimael Shemley ni mtu alie kuwa akiishi Arusha kabla hajaja Dar es salaamu alikuwa mfanya biashara mkubwa sana kule Arusha alimiliki Hotel nyingi sana na alikuwa na Shule za sekondari biashara aliyo kuwa akiifanya ni kuuza wanawake na kuuza viungo vya wanawake matiti, na vitu mbalimbali kutoka katika mwili wa mwanamke huyu Ishimael Shemley alikuza wigo wa kazi akawa anauza wanawake njje ya nchi hii, kila Hoteli aliyo kuwa akimiliki pembeni yake palikuwa na sehemu wanawake walio kuwa wanajiuza, wengi wanawake na wasichana wamekufa kwa sababu ya kuumwa magonjwa ya zina kama ukimwi na mengineyo mengi, wanawake alikuwa anawapata vijijini kwa kisingizio kwamba anawachukua wasichana na kuwaajiri kwenye hoteli zake lakini baada ya kuwatoa vijijini wengine wanakufa na wengine wana potea na wengine kutoloka na kurudi nyumbani kwao wakiwa na mimba na wengi wakiwa na magonjwa kama vile ukimwi na mengineyo.
baada ya muda kadha huyu mtu alichaguliwa kuwa kiongozi na baada yakuchaguliwa alichaguliwa kuwa mbunge wa Arusha mjini na mwishoe akapewa uwaziri wa mambo ya ndani,
wengi tulidhani biashara ile angeiacha ila kumbe sawa na kuchukua moto na kuweka gesi ya kupikia.
aliendelea na biashara ya kuuza akina dada na kudhamini makundi mbalimbali ya ujambazi na wizi."
jaji alihisi kulegea baada ya kusikia hayo "heeeee kumbe pole sana, sasa kwanini ulimuua au nikwa sababu ya kuwa alikuwa anauza wanawake?" jaji aliuliza.
"Hapana nilimuua kwa sababu yeye kwa mjibu wa baba yangu anasema mama yangu ni moja kati ya watu walio kuwa wakiuzwa na Ishimael Shemley sasa baada ya kumuua mama yangu na huku baba hakuwa na uwezo wa kulipiza ndiyo sababu ya kwangu kumuua".
"du!! pole sana, je mama yako aliitwa nani?" Jesika ambae wakati wote alikuwa kimya aliuliza.
"baba alinionesha vitambulisho kuwa mama yangu si mtu wa kule Arusha bari ni mtu kutoka Kigoma alitoka kule kigoma kwa kudanganywa kuwa ameenda kule mjini kufanya kazi kwenye hoteli moja kule mjini ila baada ya kupelekwa mjini alicho ambulia ni kuuzwa na jina lake aliita Penina mtoto wa Mwasera"
jaji alistuka sana baada ya kusikia jina la Penina Mwasera.
"Penina Mwasera?"jaji aliuliza
"Ndiyo mwasera ni mtu kutoka kule kigoma aliishi kule lakini nilijalibu kwenda kule kigoma kufatilia ndugu na jama wa Mwasera sikumpata wala hata kupata mwelekeo nikabaki natapatapa nilikata tama" Eddison alisema.
kijasho kilimtoka Eddi hakuamini baada ya kulisikia jina la Penina Mwasera.
"umesema kuwa ni Penina Mwasera?". jaji aliuliza.
"ndiyo, kwani unamfahamu?"
eddi aliuliza.
"Ndiyo namjua tena namjua".
Edisoni alisema akiwa anatetemeka na machozi yakimtoka.
"namjua....namjua.... namjua
Penina Mwasera namjua kabisa namjua kabisa namjua"
jaji aliendelea kusema kwa pupa huku machozi yakichuruzika na akiwa anaria
kitendo ambacho kilimusisimua kila mmoja pale nakushangaa na kupata shauku la kujua nini kinaendelea na kumjua huyo Penina Ngware.
ITAENDELEA.........
MPENZI MSOMAJI TUKUTANE SEHEMU IJAYO INAYO ITWA HUKUMU YA HAKI.
LIKE AU COMMENT CHOCHOTE ILI NIJUE KAMA TUKO PAMOJA
.
BONYEZA HAPA